Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

KINGUNGE
Kingunge Ngombale Mwiru ‘ametoroka’ chama hicho kutokana na kile alichokieleza kimepoteza mwelekeo.

KINGUNGE AJITOA CCM

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Kingunge amesema, hatojiunga na chama chochote cha siasa “lakini kuanzia sasa mimi sio mwanachama wa CCM,” amesema.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, neno ‘mabadiliko’ lilitawala kinywa chake huku akionya kuwa, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa.
“Nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa sana lakini kwa utafiti wangu mimi mzee ni kuwa, nguvu ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Watu wajiamini zaidi na wasubiri tarehe 25 Oktoba mwaka huu,” amesema.

Akielezea namna CCM ilivyopoteza mwelekeo Kingunge amesema chama hicho kimelewa madaraka kutokana na kutawala kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ‘wananchi sasa wanataka mabadiliko.”

“Kuongoza nchi ni kama kupanda mlima, utafika mahala pumzi zinakwisha na huwezi kuendelea mbele na ukijaribu kwenda mbele unabaki pale pale, na hivi ndivyo CCM ambapo kimeishiwa pumzi na kimebaki pale pale hakiwezi tena kupanda mlima,” amesema Kingunge.
“Nilipigana nikiwa ndani ya CCM kuangalia nani anafaa ili kuileta nchi kwenye mstari. Niliangalia ili kujua ndani ya chama nani tukimpata anaweza kuipeleka nchi mbio.

“Nilimwona Edward Lowassa kuwa ana sifa kuliko wengi waliojitokeza. Kiongozi lazima akubalike na watu, hii ni sifa tangu wakati wa TANU,”amesema Kingunge na kuongeza;
“Lowassa anakubalika ndani ya CCM na nje ya CCM, ni hivyo pamoja na kutangaziwa mambo ya ajabu kwa miaka minane mfululizo.”
Amesema “kauli zinazotoka sasa hivi, wapinzani hawawezi kushinda. Nyinyi mnajuaje kama hawawezi kushinda? Ukiritimba wa chama kimoja kwa karne moja umetosha, madaraka hulevya.”

Akizungumiza chama tawala kuacha utamaduni wake Kingunge amesema chama hicho kimeacha ‘itikio’ lake lililoasisiwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
“Wamebadilisha kauli mbiu ya chama badala ya kidumu Chama Cha Mapinduzi – kidumu, sasa wanaitikia kidumu chama tawala,” anasema na kuongeza; “niliwaambia NEC kwamba ukisema hivyo maana yake wewe unataka kubaki kwenye utawala.”

Kingunge amzungumzia Magufuli

Akimzungumzia mgombea urasi wa CCM, Dk. John Magufuli, Kingunge amesema nafasi hiyo ameipata kutokana na chama hicho kuvunja katiba ya chama.
Hata hivyo ameeleza kuwa, tatizo kubwa la wananchi ni uchumi na ajira, “umasikini uanondolewa na uchumi bora,” amesema.

Amesema, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliacha uchumi ukikua kwa asilimia saba na kuingiza nchi kwenye orodha ya nchini zinazokwenda mbio kiuchumi.
“Tazama, Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) kapokea uchumi ukikuwa kwa silimia saba na sasa ni miaka 10 uchumi unakuwa karibu na asilimia saba -miaka 10 hii yote tumepiga make time na kiukweli tumerudi nyuma. Mabadiliko ni muhimu ili upate watu wengine wenye pumzi mpya,” amesema.

Mathias Chikawe

Waziri wa Mambo ya ndani ni miongoni mwa wanachama maarufu wa CCM walioshindwa kupita katika kura za maoni. Mathias Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyekuwa akiwania kupitishwa tena kugombea tena ubunge wa Nachingwea.

Chikawe ambaye pia alishindwa katika kinyang’anyiro cha urais kupitia chama hicho, alidondoshwa na Hassan Masala aliyepata kura 6,494 akifuatiwa naye akipata 5,128.
Mbali ya Chikawe pia manaibu waziri wanne wameangushwa katika kura hizo. Hao ni Mahadhi Juma Maalim (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Perera Ame Silima (Mambo ya Ndani), Amos Makala (Maji) na Saning’o ole Telele (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).

Mahadhi Juma Maalim

Mahadhi alianguka katika Jimbo la Paje, Zanzibar kwa kupata kura 1,785 huku Jaffar Sanya Jussa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa kusini akiibuka mshindi kwa kura 3,368.

Perera Ame Silima

Silima aliyepata kura 1,218 katika Jimbo la Chumbuni alibwagwa na mpinzani wake, Ussi Pondeza aliyepata kura 1,952.

Dkt. Milton Makongoro Mahanga ajiunga CHADEMA

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa CCM jimbo la Segerea anayemaliza muda wake, Dkt. Milton Makongoro Mahanga naye ameshindwa katika kura za maoni, na hatimae kutangaza kuhamia CHADEMA.

Dkt. Mahanga ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari akiwa nyumbani kwake Segerea mwisho, ambapo amesema ameamua kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na (CHADEMA) baada ya kushuhudia mbinu chafu zilizotumia na baadhi ya wagombea dhidi yake.

Amos Makala

Katika Jimbo la Mvomero, Suleiman Murad alishinda kwa kura 13,165 dhidi ya Makalla ambaye alikuwa anatetea jimbo hilo akipata 10,973. Ambaye yupo katika Wizara ya Maji.

Saning’o ole Telele

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Ole Telele alipata kura 5, 126 huku William ole Nasha akiibuka mshindi kwa kura 23, 563 akifuatiwa na Elias Ngolisa aliyepata 11, 442 na Dk Eliamani Lalkaita 7,135. Matokeo hayo hayakujumlisha kura za matawi matano ambayo Katibu wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Elihudi Shemauya alisema hayawezi kubadili matokeo.

Abdul Mteketa

Katika jimbo la Kilombero: Mbunge wa jimbo hilo, Abdul Mteketa alianguka baada ya kushika nafasi ya tatu kwa kupata kura 2,646 nyuma ya Abubakar Assenga aliyepata kura 6,629 na Abdul Liana 3,999.

Muhammed Seif Khatib

Katika Jimbo la Uzini, Muhammed Seif Khatib ameshindwa baada ya kupata  kura 1,333 huku mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani akiibuka kidedea kwa kura 1,521.
Wagombea wengine ni Steven Nyoni (1,438), Amandus Chinguile (1,274), Fadhili Liwaka (1,171), Benito Ng’itu (797), Greyson Francis (671), Albert Mnali (763), Issa Mkalinga (466), Mustafa Malibiche (427) na Ali Namnjundu (319).

Yahya Kassim Issa

Jimbo la Chwaka mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20,  Yahya Kassim Issa aliangushwa baada ya kupata kura 1,572 dhidi ya mpinzani wake, Baguwanji Mensuriya Baguwanji aliyepata kura 1,951.

Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha mkoba wenye Fomu za kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 23, 2015, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.

Seif Sharif Hamad, Edward Lowassa
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisoma taarifa ya muongozo kwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa kuchukua Fomu ya kuwania nafasi hiyo, kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani, Zanzibar. Maalim Seif alisindikizwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,Mgombea Mweza, Dkt. Juma Haji Duni pamoja na viongozi wengine wanaounda UKAWA.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mhe. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na NCCR-Mageuzi, moja ya chama kati ya vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Sumaye anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kuhama chama tawala, CCM, kama alivyofanya Edward Lowassa, ambaye naye alitangaza kujiunga CHADEMA mwezi Julai baada ya kutokuridhishwa na mchujo wa kupata mgombea Urais wa Tanzania 2015 na kufanikiwa kuteuliwa na chama chake kipya kuwakilisha vyama vinne katika kiti hicho.
Akitangaza uamuzi wake huo moja kwa moja "LIVE" kupitia runinga ya ITV katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi.

Amesema kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hichowaliokuwa wakizunguka nchi nzima walijielekeza zaidi kuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura.
Sumaye amesema kuwa, "kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli" na kuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakisha mabadiliko hayo.

Majimbo hayo yalitangazwa na wawakilishi wa makatibu wakuu wa UKAWA, John Mnyika (Chadema), Nderakindo Kessy (NCCR – Mageuzi), Shaweji Mketo (CUF) na Masudi Makujunga (NLD) waliokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya za NCCR – Mageuzi.

Majimbo waliogawana UKAWA

253 ni majimbo ambayo yamegawanywa na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kati ya majimbo 265 ya ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano yakibaki kiporo.
John Mnyika (Chadema), Nderakindo Kessy (NCCR – Mageuzi), Shaweji Mketo (CUF) na Masudi Makujunga (NLD)

Majimbo ya UKAWA

Miongoni mwa majimbo ambayo hayajagawanywa ni, Segerea, Kigamboni, Mbarali, Geita Vijijini, Gairo, Mtwara, Mpwapwa na Geita Mjini, Mwanga na Serengeti ambalo Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe jana alichukua fomu kuliwania.

Katika mgawanyo huo uliotangazwa kwa wanahabari jana, Chadema kimepata majimbo 138, sawa na asilimia 73 ya majimbo yote huku CUF ikichukua majimbo 99, NCCR – Mageuzi majimbo 14 na NLD majombo matatu.
Hiyo ni pamoja na kujumlisha majimbo 51 ya Zanzibar ambayo yote yalikwenda kwa CUF isipokuwa moja lililoachwa kwa Chadema.

Takwimu za Uchaguzi

Chadema ambacho katika uchaguzi uliopita kilipata majimbo 24 dhidi ya manne ya NCCR-Mageuzi na mawili ya CUF Bara, kimeachiwa majimbo karibu yote katika mikoa ya Mara, Shinyanga, Geita, Njombe, Rukwa, Arusha, Manyara, Singida, Katavi huku Cuf ikibeba mkoa wote wa Lindi na NCCR-Mageuzi ikibeba ngome ya Kigoma.
Katika mgawanyo huo, NLD ambayo haikuwa na jimbo hata moja imeachiwa majimbo matatu tu ya Lulindi, Masasi na Ndanda mkoani Mtwara.

Wawakilishi wa makatibu wakuu wa UKAWA walisema uamuzi huo umefikiwa baada ya majadiliano ya muda mrefu, kuhusu kuachiana majimbo ya ubunge kwa vyama vinavyounda UKAWA.

Dk Titus Kamani ashindwa uchaguzi

Hali ilikuwa mbaya jimboni Busega ambako baada ya Dk Kamani na wafuasi walizuia matokeo kutangazwa na kuibuka kwa vurugu zilizosababisha polisi kuingilia kati na kukamata watu wanne walioonekana kumuunga mkono.

Matokeo ya Jimbo la Busega yamekwama baada ya Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk Titus Kamani kumshambulia msimamizi wa uchaguzi, baada ya kutangazwa matokeo kua ameshindwa.

Mawaziri wengine walioshindwa, Bofya hapa

Dk. Chegeni ambwaga Dk.Kamani

Halmashauri Kuu ya CCM iliagiza kurudiwa kwa kura za maoni za ubunge kwenye jimbo hilo baada ya kubaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni. Katika kura za Awali, Dk Kamani na Dk Chegeni, kila mmoja kwa wakati wake alijitangaza kuwa mshindi, lakini baada ya matokeo rasmi kutangaza Dk Chegeni aliibuka mshindi kwa kupata kura 13,048 dhidi ya 11,829 za Dk Kamani.


“Napigania haki yangu,” alisema Dk Kamani baada ya kutulia kwa vurugu ambazo zilihusisha kupigwa kwa msimamizi wa kura hizo za maoni, Jonathan Mabiya.
“Huu ni ushindani. Uchaguzi uliopita tulikubaliana na matokeo na tulisaini, lakini uongozi umesema turudie, leo hatujasaini wanataka kutangaza kwa nguvu, hatujakubaliana.”

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, licha ya matokeo kutotatangazwa alisema watu hawana budi kukubaliana na matokeo na kusema kitendo cha Dk Kamani kwa kuhusika kwenye vurugu hizo ni cha kibinadamu.

“Aliyeshinda ameshinda tu hakuna namna. Kilichofanywa na Waziri Kamani kumpiga msimamizi huyo ni mambo ya binadamu tu… lakini walioshindwa lazima wakubali matokeo na lazima yatangazwe,” alisema Mzindakaya.


Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, wamepokelewa kwa kishindo jijini Mwanza ikielezwa kuwa idadi ya watu waliojitokeza kumlaki mgombea huyo ni mara dufu ya wale waliojitokeza mikoa ya Dar, Mbeya na Arusha.



Wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo uwanja wa ndege wa Mwanza, Jeshi la Polisi lililazimika kuwatawanya watu kwa kutumia mabomu ya machozi kutokana na msululu mkubwa wa watu waliokuwa wanataka kuingia eneo la uwanja wa ndege.

habari za Lowassa

LIPUMBA AJIONDOA UKAWA

Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekua mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) alitangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.

Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.

Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

Lowassa ajiunga Chadema

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema umemkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kujiunga nao katika harakati za kuking'oa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mbatia akimuongelea Lowassa

Mbatia: Tunamkaribisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward Ngoyaye Lowasa kujiunga na UKAWA, ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.

Mbatia: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri.

Lipumba juu ya Lowassa

"Lowasa alishasema yeyote mwenye ushahidi aulete..hapa tumekaribisha Watanzania wote kujiunga. Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.

Endelea kutembelea hapa kwa habari za kina na uhakika.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda

UPINZANI KUCHUKUA DOLA

Chama chochote cha siasa nchini kina nafasi ya kushika dola endapo kitafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika, alisema Waziri Mkuu msataafu Dk. Salim Ahmed Salim
Waziri mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim  akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa Semina ya Urithi na Utamaduni wa Tanzania. Kushoto ni mkurugenzi wa taasisi hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM), Profesa Abdallah Bujra
“Utakuta viongozi wa vyama wenyewe kwa wenyewe wanarushiana maneno, huyu hafai  mara siyo raia wa nchi hii, sasa haya mambo kwenye siasa hayatakiwi.

“Ni lazima kila kiongozi wa chama cha siasa atambue wajibu  wake katika jamii,”
Pia maadili ya viongozi katika Taifa yameporomoka,  hivyo aliwaasa wananchi kuchagua viongozi bora kwa masilahi ya Taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

“Sasa kiongozi anagombea nafasi fulani kwa masilahi yake binafsi, siyo kwa wananchi  na anawaomba wampigie kura,” alisema Dk Salim.
Dk Salim alisema hayo jana baada ya kufungua semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Utamaduni na Urithi kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).
Aliwataka wananchi kuwa watulivu  na kuilinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Katika semina hiyo ya Urithi na Utamaduni wa Tanzania alisema nchi ina urithi lakini haujapewa kipaumbele.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Profesa Abdallah Bujra alisema semina hiyo itakuwa ya siku tatu.

Alisema Taifa haliwezi kupiga hatua bila suala hilo kutiliwa mkazo.

Aliyekua Mbunge wa Viti Maalu, Ester Bulaya ametangaza kutokugombea Ubunge kupitia CCM.

Jimbo la Bunda Mjini

Mchuano unatarajiwa kuwapo katika Jimbo la Bunda Mjini ambako Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira atavaana na aliyekua Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya.

Wabunge hao wa CCM wamekuwa wakitambiana muda mrefu na wakati mwingine waliwahi kurushiana maneno hadi bungeni, lakini mwisho wa tambo zote ni kwenye kura za maoni.



Vijana wanao aminika kua ni wafuasi wa Lowassa wahamia CHADEMA.





Joseph Butiku,Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere
Joseph Butiku,Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere
Joseph Butiku,Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere amesema nchi inaongozwa na Katiba, lakini inashangaza viongozi wa chama chake cha CCM na vingine ndiyo wanaongoza kwa kuvunja sheria na taratibu.

“Huko nyuma kulikuwa na matatizo, lakini sasa chama changu (CCM) na vyama vingine ndiyo magwiji wa kuvunja taratibu,” alisema Butiku wakati akichangia hoja jana kwenye mdahalo wa umuhimu wa Kulinda Amani na Umoja uliorushwa moja kwa moja na ITV.

“Mtandao huo iliamua kufanya kazi nje ya CCM kwa sababu itikadi zao na sisi zilitofautiana. Eti wanasema CCM ni chama cha mizengwe kinawachelewesha kutajirika. Sasa hao watu ndiyo wameendelea kuwapo na kusababisha haya matatizo yaendelee,” alisema Butiku.

“Kama baadhi wa watu muhimu wapo nje, sasa mwenyekiti wetu (Rais Jakaya Kikwete) amekwenda kufanya nini huko? Kama viongozi wa CCM wameshampata mtu wanayemtaka (kugombea urais) wanakwenda Dodoma kufanya nini. Huku si kumkejeli Rais Kikwete?” alihoji.

Alisema viongozi hawafuati utaratibu, kila kitu lazima hela. “Sasa tunatoka kwenye utaratibu wetu wa vyama tunashiriki katika kufanya uovu. Kama haki inauzwa, hatuwezi kupata amani. Viongozi wanatoa rushwa hata kabla ya kupewa nchi. Je, wakipewa nchi itakuwaje?” alihoji.

ACT-TANZANIA, ACT-WAZALENDO
ACT-TANZANIA

ACT-TANZANIA DHIDI YA ACT-WAZALENDO

ACT-WAZALENDO, ACT-TANZANIA
ACT-WAZALENDO
Zitto alijiunga ACT-TANZANIA

Mwenyekiti wa ACT-TANZANIA
Mkuu wa Chama wa ACT-WAZALENDO

NINI TOFAUTI YA ACT-TANZANIA NA ACT-WAZALENDO ?
KARIBU TUPE MAONI YAKO

ACT-TANZANIA
ZITTO KABWE
Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Kauli ya hiyo ya Bunge imekuja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kumvua uanachama Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema kutokana na hali hiyo, Zitto bado ni mbunge halali wa Kigoma Kaskazini na kwamba anapaswa kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria. Dk Thomas Kashililah, amebainisha kuwa endapo Bunge litapata taarifa rasmi ya Chadema kumvua uanachama Zitto, lazima Bunge hilo lifanye kwanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndipo litoe uamuzi.

Pia amesema sakata la mbunge wa Bunge hilo kuvuliwa uanachama na chama chake si la kwanza, kwani tayari kuna mbunge aliyevuliwa uanachama na chama chake lakini Bunge hilo halikumvua uanachama wake baada ya kumaliza uchunguzi wake. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo. “Utaratibu ulivyo, chama huliandikia Bunge kuhusu kumvua uanachama mbunge na Bunge kabla ya uamuzi wowote hufuatilia kwanza sababu za kuvuliwa uanachama huo, ili kujiridhisha kama zilikuwa halali au la,” alisema Kashililah.

Alisema baada ya hapo Bunge hilo huwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili ofisi hiyo ya msajili iweze kupitia Katiba ya chama husika na kupitia sababu za chama husika zinazoweza kumvua uanachama mwanachama wake na kama kweli zimekiukwa.

“Baada ya suala hilo kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, Spika wa Bunge, hutoa uamuzi baada ya kuchunguza na uamuzi huo, hupelekwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi,”alisisitiza.

Aidha alisisitiza: “Si lazima Spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa mbunge husika kwani kama haikuwa halali kwa mbunge huyo kuvuliwa uanachama, Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika,” alisema.

Alisema Spika Anne Makinda katika kipindi chake alishawahi kutoa uamuzi wa kubatilisha mbunge fulani kuvuliwa ubunge hata baada ya chama chake kumvua uanachama.

Akizungumzia suala hilo, Zitto, alisema kwa upande wake bado ni mbunge na anaendelea na kazi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) hadi pale atakapopatiwa taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na ubunge wake.

“Naendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea, sina taarifa yoyote ya kuvuliwa uanachama wangu wala ubunge, habari hizi nimezisikia kwenye vyombo vya habari, sijaitwa na Mahakama kuambiwa kinachoendelea,”alisema Zitto.

Alisema kwa sasa anaendelea kuongoza kamati hiyo na jana alikutana na menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo kamati yake inatarajia kukutana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watakutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwanasheria Mkuu kuhusu mapato ya akaunti za madini.

Aidha alisema pamoja na kuendelea kama kawaida na shughuli zake za kibunge bungeni, pia anatarajia kesho kwenda Kigoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo jimboni kwake, kabla ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza rasmi Machi 17, mwaka huu.

Alisema kwa upande wake, anachukulia suala hilo kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika medani za siasa nchini na duniani kote.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama hicho kinajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, ikiwemo kuandaa na kuiwasilisha wakati wowote barua inayomvua uanachama Zitto, ili suala hilo lifanyiwe uamuzi mapema.

“Kwa sasa suala hili la Zitto limewaingia Watanzania wengi, sasa sisi tunataka tulifanyie kazi mapema, ili uamuzi ufanywe mapema na suala hili liishe. Kuna mambo mengi ya maana yanahitaji kujadiliwa kitaifa kama vile masuala ya uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa BVR,” alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye juzi alitangaza kuwa chama hicho kimemvua uanachama mbunge huyo, jana alimwambia mwandishi kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho litaifikisha taarifa ya Zitto kuvuliwa uanachama kwa Kamati Kuu ya chama ifikapo Mei, mwaka huu.

Alisema, "Kutokana na utaratibu uliopangwa wa Kamati Kuu kukutana kila baada ya miezi mitatu, suala la Zitto litasubiri kikao kingine cha kawaida cha kamati hiyo kitakachokaa mwezi Mei. Kikao kilichopita kilikaa Februari mwaka huu".

Kwa maelezo ya Lissu, baada ya hapo ndipo wataiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuijulisha kuwa Zitto si mwanachama wa chama hicho tena au la.

ZITTO KABWE
Siasa za Tanzania kwa hivi sasa zimechukua mkondo mpya baada ya aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kujiunga rasmi na chama alichokuwa akihusishwa kwa muda mrefu, chama cha ACT-Tanzania.

SAMSONI MWIGAMBA AKITETA JAMBO NA ZITTO KABWE
Mwanasiasa huyo ambaye jana alikutana na waandishi wa habari na kueleza sababu za kujiunga na chama hicho amekuwa akijadiliwa katika kona mbalimbali kutokana na hatua yake hiyo ambayo wengine wanaitizama kama ni hatua itakayokoleza ushindani mkali kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao.

Miongoni mwa watu wanaotajwa kuasisi chama hicho kipya ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia amewahi kuwa kiongozi ndani ya CHADEMA kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kuandaa mkakati wa kuleta mapinduzi katika chama hicho.

Profesa Kitila Mkumbo akiwa na Zitto Kabwe
Wapo watu wengi maarufu wameshajiunga na chama cha ACT- Tanzania kama orodha hapa chini inavyoonyesha:
Orodha ya baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Tanzania
Msanii maarufu kwa jina la AFANDE SELE
Una maoni gani kuhusu uwepo wa chama hicho kipya katika uwanja wa siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Toa maoni yako sasa na mshirikishe mwenzako habari hii.

Ujumbe wa Dk.Slaa kutoka Kigoma

Katika maandamano yaliyofanyika Kigoma, na huu ndio Ujumbe kwa Dk.Slaa.

Wana Habari Duniani mnatoa maoni gani?

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE