ZITTO KABWE |
Siasa
za Tanzania kwa hivi sasa zimechukua mkondo mpya baada ya aliyekuwa mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kujiunga rasmi na chama alichokuwa akihusishwa
kwa muda mrefu, chama cha ACT-Tanzania.
SAMSONI MWIGAMBA AKITETA JAMBO NA ZITTO KABWE |
Mwanasiasa huyo ambaye jana alikutana na waandishi wa habari na kueleza sababu
za kujiunga na chama hicho amekuwa akijadiliwa katika kona mbalimbali kutokana
na hatua yake hiyo ambayo wengine wanaitizama kama ni hatua itakayokoleza
ushindani mkali kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi
mkuu ujao.
Miongoni mwa watu wanaotajwa kuasisi chama hicho kipya ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia amewahi kuwa kiongozi ndani ya CHADEMA kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kuandaa mkakati wa kuleta mapinduzi katika chama hicho.
Profesa Kitila Mkumbo akiwa na Zitto Kabwe |
Wapo watu wengi maarufu wameshajiunga na chama cha ACT- Tanzania kama orodha hapa chini inavyoonyesha:
Orodha ya baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Tanzania |
Msanii maarufu kwa jina la AFANDE SELE |
Una maoni gani kuhusu
uwepo wa chama hicho kipya katika uwanja wa siasa za vyama vingi nchini
Tanzania. Toa maoni yako sasa na mshirikishe mwenzako habari hii.
Tweet