Mapenzi |
Msifie
Kila
siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila
msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini
kuliko msichana yeyote awaye.
Muandikie
Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg
kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda
kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu
katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe
msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.
Mbusu
Busu
la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia
raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi
humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya
kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali
Fanyika kua msaada
Tambua
mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa
pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa
sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia
katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa
lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana
anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida
nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.
Mtoko Muhimu
Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.Kua muwazi kwake
Kuwa
muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa
mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona
umemuamini
Usiwe Busy Kupitiliza
Ukijiona
upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama
ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha
unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.
Mkumbatie
Mkumbatie
mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake
tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale
msipokuwa pamoja.
Staarabika
Epuka
maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa
mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza
unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na
wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.
Mdekeze
Msichana
anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana
ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa
kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku
nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo
silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana.
Tweet