Lowassa ajiunga Chadema
Umoja
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema umemkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu
Mhe. Edward Lowassa kujiunga nao katika harakati za kuking'oa Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Mbatia akimuongelea Lowassa
Mbatia:
Tunamkaribisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward Ngoyaye Lowasa
kujiunga na UKAWA, ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio
tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa
lazima. Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.
Mbatia:
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo)
tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri.
Lipumba juu ya Lowassa
"Lowasa alishasema yeyote mwenye ushahidi aulete..hapa tumekaribisha
Watanzania wote kujiunga. Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua
bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote
atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi
haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.
Endelea
kutembelea hapa kwa habari za kina na uhakika.
Tweet