Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
UPINZANI KUCHUKUA DOLA
Chama
chochote cha siasa nchini kina nafasi ya kushika dola endapo kitafuata kanuni
na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika, alisema Waziri Mkuu msataafu Dk.
Salim Ahmed Salim
“Utakuta
viongozi wa vyama wenyewe kwa wenyewe wanarushiana maneno, huyu hafai
mara siyo raia wa nchi hii, sasa haya mambo kwenye siasa hayatakiwi.
“Ni
lazima kila kiongozi wa chama cha siasa atambue wajibu wake katika jamii,”
Pia
maadili ya viongozi katika Taifa yameporomoka, hivyo aliwaasa wananchi
kuchagua viongozi bora kwa masilahi ya Taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25
mwaka huu.
“Sasa
kiongozi anagombea nafasi fulani kwa masilahi yake binafsi, siyo kwa
wananchi na anawaomba wampigie kura,” alisema Dk Salim.
Dk
Salim alisema hayo jana baada ya kufungua semina iliyoandaliwa na Taasisi ya
Utamaduni na Urithi kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).
Aliwataka
wananchi kuwa watulivu na kuilinda amani katika kipindi hiki cha
uchaguzi.
Katika
semina hiyo ya Urithi na Utamaduni wa Tanzania alisema nchi ina urithi lakini
haujapewa kipaumbele.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo, Profesa Abdallah Bujra alisema semina hiyo itakuwa ya siku
tatu.
Alisema
Taifa haliwezi kupiga hatua bila suala hilo kutiliwa mkazo.
Tweet