Majimbo
hayo yalitangazwa na wawakilishi wa makatibu wakuu wa UKAWA, John Mnyika
(Chadema), Nderakindo Kessy (NCCR – Mageuzi), Shaweji Mketo (CUF) na Masudi
Makujunga (NLD) waliokutana katika Ofisi za Makao Makuu ya za NCCR – Mageuzi.
Majimbo waliogawana UKAWA
253
ni majimbo ambayo yamegawanywa na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kati ya majimbo 265 ya ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano
yakibaki kiporo.
Majimbo ya UKAWA
Miongoni
mwa majimbo ambayo hayajagawanywa ni, Segerea, Kigamboni, Mbarali, Geita
Vijijini, Gairo, Mtwara, Mpwapwa na Geita Mjini, Mwanga na Serengeti ambalo
Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi, Mosena Nyambabe jana alichukua fomu kuliwania.
Katika
mgawanyo huo uliotangazwa kwa wanahabari jana, Chadema kimepata majimbo 138,
sawa na asilimia 73 ya majimbo yote huku CUF ikichukua majimbo 99, NCCR –
Mageuzi majimbo 14 na NLD majombo matatu.
Hiyo
ni pamoja na kujumlisha majimbo 51 ya Zanzibar ambayo yote yalikwenda kwa CUF
isipokuwa moja lililoachwa kwa Chadema.
Takwimu za Uchaguzi
Chadema
ambacho katika uchaguzi uliopita kilipata majimbo 24 dhidi ya manne ya
NCCR-Mageuzi na mawili ya CUF Bara, kimeachiwa majimbo karibu yote katika mikoa
ya Mara, Shinyanga, Geita, Njombe, Rukwa, Arusha, Manyara, Singida, Katavi huku
Cuf ikibeba mkoa wote wa Lindi na NCCR-Mageuzi ikibeba ngome ya Kigoma.
Katika
mgawanyo huo, NLD ambayo haikuwa na jimbo hata moja imeachiwa majimbo matatu tu
ya Lulindi, Masasi na Ndanda mkoani Mtwara.
Wawakilishi wa makatibu wakuu wa UKAWA walisema uamuzi huo umefikiwa baada ya majadiliano ya muda
mrefu, kuhusu kuachiana majimbo ya ubunge kwa vyama vinavyounda UKAWA.
Tweet