Mathias Chikawe
Waziri
wa Mambo ya ndani ni miongoni mwa wanachama maarufu wa CCM walioshindwa kupita
katika kura za maoni. Mathias Chikawe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
aliyekuwa akiwania kupitishwa tena kugombea tena ubunge wa Nachingwea.
Chikawe
ambaye pia alishindwa katika kinyang’anyiro cha urais kupitia chama hicho,
alidondoshwa na Hassan Masala aliyepata kura 6,494 akifuatiwa naye akipata
5,128.
Mbali
ya Chikawe pia manaibu waziri wanne wameangushwa katika kura hizo. Hao ni
Mahadhi Juma Maalim (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Perera Ame
Silima (Mambo ya Ndani), Amos Makala (Maji) na Saning’o ole Telele (Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi).
Mahadhi Juma Maalim
Mahadhi
alianguka katika Jimbo la Paje, Zanzibar kwa kupata kura 1,785 huku Jaffar
Sanya Jussa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa kusini akiibuka
mshindi kwa kura 3,368.
Perera Ame Silima
Silima
aliyepata kura 1,218 katika Jimbo la Chumbuni alibwagwa na mpinzani wake, Ussi
Pondeza aliyepata kura 1,952.
Dkt. Milton Makongoro Mahanga ajiunga CHADEMA
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa CCM jimbo la Segerea anayemaliza muda wake, Dkt. Milton Makongoro Mahanga naye ameshindwa katika kura za maoni, na hatimae kutangaza kuhamia CHADEMA.
Dkt. Mahanga ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari
akiwa nyumbani kwake Segerea mwisho, ambapo amesema ameamua kuachana na Chama
cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na (CHADEMA) baada ya kushuhudia mbinu chafu
zilizotumia na baadhi ya wagombea dhidi yake.
Amos Makala
Katika
Jimbo la Mvomero, Suleiman Murad alishinda kwa kura 13,165 dhidi ya Makalla
ambaye alikuwa anatetea jimbo hilo akipata 10,973. Ambaye yupo katika Wizara ya Maji.
Saning’o ole Telele
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Ole
Telele alipata kura 5, 126 huku William ole Nasha akiibuka mshindi kwa kura 23,
563 akifuatiwa na Elias Ngolisa aliyepata 11, 442 na Dk Eliamani Lalkaita
7,135. Matokeo hayo hayakujumlisha kura za matawi matano ambayo Katibu wa CCM
Wilaya ya Ngorongoro, Elihudi Shemauya alisema hayawezi kubadili matokeo.
Abdul Mteketa
Katika jimbo la Kilombero:
Mbunge wa jimbo hilo, Abdul Mteketa alianguka baada ya kushika nafasi ya tatu
kwa kupata kura 2,646 nyuma ya Abubakar Assenga aliyepata kura 6,629 na Abdul
Liana 3,999.
Muhammed Seif Khatib
Katika
Jimbo la Uzini, Muhammed Seif Khatib ameshindwa baada ya kupata kura
1,333 huku mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani akiibuka kidedea kwa kura 1,521.
Wagombea
wengine ni Steven Nyoni (1,438), Amandus Chinguile (1,274), Fadhili Liwaka
(1,171), Benito Ng’itu (797), Greyson Francis (671), Albert Mnali (763), Issa
Mkalinga (466), Mustafa Malibiche (427) na Ali Namnjundu (319).
Yahya Kassim Issa
Jimbo
la Chwaka mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20, Yahya Kassim Issa
aliangushwa baada ya kupata kura 1,572 dhidi ya mpinzani wake, Baguwanji
Mensuriya Baguwanji aliyepata kura 1,951.
Tweet