KINGUNGE AJITOA CCM
Akizungumza
na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Kingunge
amesema, hatojiunga na chama chochote cha siasa “lakini kuanzia sasa mimi sio
mwanachama wa CCM,” amesema.
Katika
mazungumzo yake na waandishi wa habari, neno ‘mabadiliko’ lilitawala kinywa
chake huku akionya kuwa, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa.
“Nguvu
ya kupinga mabadiliko ni kubwa sana lakini kwa utafiti wangu mimi mzee ni kuwa,
nguvu ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Watu wajiamini zaidi na wasubiri
tarehe 25 Oktoba mwaka huu,” amesema.
Akielezea
namna CCM ilivyopoteza mwelekeo Kingunge amesema chama hicho kimelewa madaraka
kutokana na kutawala kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ‘wananchi sasa wanataka
mabadiliko.”
“Kuongoza
nchi ni kama kupanda mlima, utafika mahala pumzi zinakwisha na huwezi kuendelea
mbele na ukijaribu kwenda mbele unabaki pale pale, na hivi ndivyo CCM ambapo
kimeishiwa pumzi na kimebaki pale pale hakiwezi tena kupanda mlima,” amesema Kingunge.
“Nilipigana
nikiwa ndani ya CCM kuangalia nani anafaa ili kuileta nchi kwenye mstari.
Niliangalia ili kujua ndani ya chama nani tukimpata anaweza kuipeleka nchi
mbio.
“Nilimwona
Edward Lowassa kuwa ana sifa kuliko wengi waliojitokeza. Kiongozi lazima
akubalike na watu, hii ni sifa tangu wakati wa TANU,”amesema Kingunge na kuongeza;
“Lowassa
anakubalika ndani ya CCM na nje ya CCM, ni hivyo pamoja na kutangaziwa mambo ya
ajabu kwa miaka minane mfululizo.”
Amesema “kauli
zinazotoka sasa hivi, wapinzani hawawezi kushinda. Nyinyi mnajuaje kama
hawawezi kushinda? Ukiritimba wa chama kimoja kwa karne moja umetosha, madaraka
hulevya.”
Akizungumiza
chama tawala kuacha utamaduni wake Kingunge amesema chama hicho kimeacha ‘itikio’
lake lililoasisiwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
“Wamebadilisha
kauli mbiu ya chama badala ya kidumu Chama Cha Mapinduzi – kidumu, sasa
wanaitikia kidumu chama tawala,” anasema
na kuongeza; “niliwaambia NEC kwamba ukisema hivyo maana yake wewe
unataka kubaki kwenye utawala.”
Kingunge amzungumzia Magufuli
Akimzungumzia
mgombea urasi wa CCM, Dk. John Magufuli, Kingunge amesema nafasi hiyo ameipata
kutokana na chama hicho kuvunja katiba ya chama.
Hata
hivyo ameeleza kuwa, tatizo kubwa la wananchi ni uchumi na ajira, “umasikini
uanondolewa na uchumi bora,” amesema.
Amesema,
Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliacha uchumi ukikua kwa asilimia saba
na kuingiza nchi kwenye orodha ya nchini zinazokwenda mbio kiuchumi.
“Tazama,
Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) kapokea uchumi ukikuwa kwa silimia saba na sasa
ni miaka 10 uchumi unakuwa karibu na asilimia saba -miaka 10 hii yote tumepiga
make time na kiukweli tumerudi nyuma. Mabadiliko ni muhimu ili upate watu
wengine wenye pumzi mpya,” amesema.