Dk Titus Kamani ashindwa uchaguzi

Hali ilikuwa mbaya jimboni Busega ambako baada ya Dk Kamani na wafuasi walizuia matokeo kutangazwa na kuibuka kwa vurugu zilizosababisha polisi kuingilia kati na kukamata watu wanne walioonekana kumuunga mkono.

Matokeo ya Jimbo la Busega yamekwama baada ya Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk Titus Kamani kumshambulia msimamizi wa uchaguzi, baada ya kutangazwa matokeo kua ameshindwa.

Mawaziri wengine walioshindwa, Bofya hapa

Dk. Chegeni ambwaga Dk.Kamani

Halmashauri Kuu ya CCM iliagiza kurudiwa kwa kura za maoni za ubunge kwenye jimbo hilo baada ya kubaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni. Katika kura za Awali, Dk Kamani na Dk Chegeni, kila mmoja kwa wakati wake alijitangaza kuwa mshindi, lakini baada ya matokeo rasmi kutangaza Dk Chegeni aliibuka mshindi kwa kupata kura 13,048 dhidi ya 11,829 za Dk Kamani.


“Napigania haki yangu,” alisema Dk Kamani baada ya kutulia kwa vurugu ambazo zilihusisha kupigwa kwa msimamizi wa kura hizo za maoni, Jonathan Mabiya.
“Huu ni ushindani. Uchaguzi uliopita tulikubaliana na matokeo na tulisaini, lakini uongozi umesema turudie, leo hatujasaini wanataka kutangaza kwa nguvu, hatujakubaliana.”

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, licha ya matokeo kutotatangazwa alisema watu hawana budi kukubaliana na matokeo na kusema kitendo cha Dk Kamani kwa kuhusika kwenye vurugu hizo ni cha kibinadamu.

“Aliyeshinda ameshinda tu hakuna namna. Kilichofanywa na Waziri Kamani kumpiga msimamizi huyo ni mambo ya binadamu tu… lakini walioshindwa lazima wakubali matokeo na lazima yatangazwe,” alisema Mzindakaya.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE