Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mhe. Frederick Sumaye kujivua
uanachana na kujiunga na NCCR-Mageuzi, moja ya chama kati ya vinne vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Sumaye
anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kuhama chama tawala, CCM, kama alivyofanya
Edward Lowassa, ambaye naye alitangaza kujiunga CHADEMA mwezi Julai baada ya
kutokuridhishwa na mchujo wa kupata mgombea Urais wa Tanzania 2015 na
kufanikiwa kuteuliwa na chama chake kipya kuwakilisha vyama vinne katika kiti
hicho.
Akitangaza
uamuzi wake huo moja kwa moja "LIVE" kupitia runinga ya ITV katika mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam,
Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi.
Amesema
kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama
hichowaliokuwa wakizunguka nchi nzima walijielekeza zaidi kuishambulia serikali
badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura.
Sumaye
amesema kuwa, "kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli
kweli" na kuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na
upinzani ili kuharakisha mabadiliko hayo.
Tweet