Showing posts with label Mikoani. Show all posts
Showing posts with label Mikoani. Show all posts

Mapenzi

Msifie

Kila siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye. 

Muandikie 

Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako. 

Mbusu 

Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali

Fanyika kua msaada 

Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.

Mtoko Muhimu

Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.

Kua muwazi kwake

Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini

Usiwe Busy Kupitiliza

Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.

Mkumbatie

Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.

Staarabika

Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.

Mdekeze

Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana.

The government of Tanzania to implement President John Magufuli’s promise to provide 50m/- to every village for development starts in the 2016/2017 financial year, Deputy Minister in the Prime Minister’s Office, Labour, Youth and Employment, Anthony Mavunde said here yesterday.
He told the National Assembly that the procedures on the best way of distributing the money were being prepared by National Economic Empowerment Council (NEEC) together with Regional Administration and Local Government.

The deputy minister was responding to a question by Halima Bulembo (Special Seats-CCM) who wanted to know when the promise would be implemented and at what percentage of the amount would be reserved for the youths.

NEEC Executive Secretary Beng’i Issa said that the money would be released in three phases within a period of five years. She said the funds would first be released to banks before being channelled to various groups like Village Community Banks, SACCOS and Village Savings and Loan Association (VSLA) in the country according to agreed arrangement.

The MP for Buyugu on Chadema ticket, Mr Kasuku Bilango, wanted the government’s commitment to distribute the money fairly to all citizens, saying there were rumours that only members of the ruling CCM in the villages will benefit.

However, the Minister of State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled), Ms Jenista Mhagama, dismissed the sentiments as mere worries, saying all legal procedures would be followed.

She pointed out that the money was the president’s promise during his campaign for the presidency and would be distributed to all the citizens regardless of their political ideologies.

It was recently reported that the government plans to use 811bn/- in the next five years to implement the president’s promise and it has started to engage various stakeholders on how best to accomplish the task.

10 REGIONS TO RECEIVE MAGUFULI'S 50 MILLION

The plan shows that the exercise would commence in 10 regions with less financial services. The regions include Singida, Lindi, Mtwara, Mbeya, Shinyanga, Geita, Kagera, Dodoma, Rukwa and Ruvuma.

James Lembeli

James Lembeli, Mbunge wa Kahama aliyemaliza muda wake amekataa kubadili msimamo wake wa kutogombea ubunge kupitia CCM akisema atagombea nafasi hiyo kupitia chama kingine.

Akizungumza mjini hapa jana, Lembeli alisema hawezi kubadili msimamo wake wa kuondoka CCM, kutokana na masharti mazito ya kimila aliyopewa kabla ya kutangaza kuondoka katika chama hicho.

Baada ya uamuzi wake, watu mbalimbali, wakiwamo maofisa wa Serikali na wafanyabiashara waliahidi kumsaidia hata nguvu ya kifedha, wakimtaka atengue uamuzi wake achukue fomu katika Jimbo la Kahama Mjini.
Alisema hawezi kukiuka masharti ya kimila kwa kuwa yeye ni mtoto wa chifu. Mtoto huyo wa Chifu Daud Lembeli alisema kabla ya kutoa uamuzi huo alikaa na mama yake mzazi, Maria Kalembo kuanzia saa 10 jioni hadi saa nane usiku akizungumzia suala hilo hadi walipokubaliana.

Alisema baada ya mama yake kukubali na kutoa baraka za kuhama CCM, alipigiwa ngoma za kimila za Waswezi, ambazo hutumika kutoa baraka katika imani za kichifu akisema ndizo zilizohitimisha fursa za kugombea kwake ubunge kupitia chama hicho.
“Najisikia amani kubwa kuondoka CCM, kabla sijachukua uamuzi huu nilikuwa nikiishi kwa presha, hivi sasa nipo huru, niacheni tu kama ni ubunge sikuzaliwa nao na unaweza kuishi bila ubunge na maisha yakawa mazuri,” alisema Lembeli.

WASTAAFU, MISHAHARA, TAMISEMI
RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeibua ufisadi mkubwa katika mamlaka za Serikali za mitaa,mashirika ya umma na serikali kuu. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa ripoti ya ukaguzi mjini Dodoma jana,Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad alisema ukaguzi huo umefanywa katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109.
 

Alisema usimamizi wa bajeti kwa mamlaka ya Serikali za Mitaa ulibaini kuwapo upungufu wa fedha za maendeleo Sh bilioni 312. 04, Serikali kuu Sh bilioni 1.8, fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika lakini hazikutolewa ni Sh bilioni 417.
 

Fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika ni Sh 203.13, alisema.
Alisema ripoti hiyo imebaini ukiukwaji wa matumizi ya utoaji wa misamaha ya kodi, kuendelea kwa mishahara hewa, usimamizi mbovu wa mipango miji,madeni ya Serikali katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
 

Kuhusu misamaha ya kodi, Profesa Assad alisema iliyotolewa kwa mafuta yanayotumika migodini imefikia Sh bilioni 22.33 kati ya yale yaliyotakiwa kutumiwa na makampuni ya Geita Gold Mine na Resolute Tanzania Ltd na yalipeleka mafuta hayo kwa wakandarasi wasiostahili msamaha wa kodi.
 

“Matumizi ya misamaha ya kodi kwa malengo tofauti na yasiyokusudiwa na kusababisha upotevu wa Sh milioni 392.7, iliyosababishwa na Kampuni ya Kiliwarrior Expenditions Ltd. ya Arusha iliyokuwa imesamehewa kodi ya Sh milioni 465.2 kuingiza magari 28 ambako kati ya Sh milioni 465.23, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeambulia kukusanya Sh milioni 72.5.


“Misamaha ya kodi ya Sh milioni 53.4 ilitolewa kwa Kampuni ya Kilemakyao Mountain Lodge Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi na upanuzi wa hoteli katika Kijiji cha Changarawe wilayani Meatu. Kampuni hii iliagiza magari matatu kwa kutumia msamaha wa kodi wa gari moja ya Hyundai Santa.Magari mengine ni BMW X5 na Toyota Land Cruiser Prado hayakufahamika yalipo,” alisema. 


Alisema amebaini kudorora kwa uwekezaji wa Serikali kwenye makampuni mbalimbali ambako Serikali ina hisa kutokana na kuchelewa kuongeza mtaji, wakati inapohitajika kufanya hivyo kama ambavyo inataka kutokea katika benki ya NBC Ltd.


Mashirika ambayo yamegubikwa na kusuasua kwa usimamizi wa uwekezaji wa Serikali ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATC),Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambayo yote yanahitaji ruzuku kutoka serikalini.


Mashine za EFD’s
Katika ukaguzi wa malipo, CAG amebaini kampuni binafsi hazitumii mashine za elektroniki za kutolea stakabadhi na hivyo kusababisha Sh bilioni 4.4 kutokuwa na stakabadhi hizo wakati taasisi za Serikali zimefanya malipo yenye thamani ya Sh bilioni 4.6 bila kutumia mashine hizo, mbali na halmashauri 22.


“Katika suala hili, TRA ilitoza faini ya Sh milioni 440.8 kwa wafanyabiashara walioshindwa kutumia EFD’s ambako milioni Sh 72 zililipwa na hivyo kufanya bakaa ya Sh milioni 369 ambayo haikulipwa,” alisema Profesa Assad.


Mapato ya ndani
Ukaguzi wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2014, ulibaini taasisi zilizo katika mpango wa kubakiza maduhuli na hazikurejeshwa zilikuwa Sh bilioni 32.74, hivyo kuathiri utekelezaji wa kazi zilizokuwa zimepangwa na taasisi husika.


Mishahara hewa
Ukaguzi wa CAG umebaini wafanyakazi walioacha kazi na kustaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao, licha ya Serikali kuwekeza katika mfumo wa Lawson kama njia ya kudhibiti hali hiyo.


Pia fedha za makato ya mishahara yao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi kama vile Bima ya Afya, TRA na mifuko ya hifadhi ya jamii. 
Kutokana na hali hiyo mpaka sasa fedha zilizolipwa ni Sh milioni 141.4.
Alisema katika halmashauri 36, Sh bilioni 1.01 zililipwa kwa watumishi waliotoroka kazini.


Wizara ya ujenzi
Ripoti hiyo imeitaja Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Waziri Dk.John Magufuli kuwa inaongoza kwa kudaiwa na wakandarasi.
Alisema mpaka anatoa ripoti hiyo wizara hiyo inadaiwa Sh bilioni 800. 
Lakini jambo la kushangaza wizara hiyo pia imetumia Sh bilioni 250 nje ya bajeti husika.


UKAGUZI WA MIRADI
Alisema ukaguzi wa miradi ya maendeleo mwaka 2013/14 ulihusu miradi mikubwa mitano. 
Miradi hiyo ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Mfuko wa Afya (HBF), Mfuko wa Barabara (RF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na miradi mingine ambayo inatekelezwa wizara, idara na mashirika ya umma.


“Katika ukaguzi wa hesabu za halmashauri 162, tulibaini Sh 52.7 zilizoidhinishwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo hakikutolewa hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa. 
“Hii imechangia malipo yaliyocheleweshwa kulipwa mwaka wa fedha 2013/14,” alisema.


Alisema ukaguzi ulibainia fedha zilizotolewa na kutotumika ndani ya mwaka wa fedha 2013/14, ni Sh bilioni 495.9 ikiwa ni asilimia 25.45 ya fedha zote za miradi. 
“Sababu kubwa ya bakaa hii ni pamoja na ucheleweshaji wa kutoa fedha kwa wadau wa maendeleo na mchango wa Serikali, mchakato mrefu wa taratibu za ununuzi, uwezo mdogo wa halmashauri wa kutumia fedha za miradi na wafanyakazi wachache wenye utaalamu katika kusimamia fedha za miradi.


Ocean Road
Alisema Taasisi ya Ocean Road inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa wa kansa.
“Mahitaji halisi ni mashine 36, wakati zilizopo ni mashine 11 tu ambazo kati ya hizo, mashine tatu zimeshapitwa na wakati zinangoja kuondolewa na mashine nne zinahitaji kufanyiwa ukarabati.


“Hali hiyo inasababisha ucheleweshaji wa matibabu hususan mionzi kwa wagonjwa ambako humchukua mgonjwa zaidi ya miezi mitatu kutibiwa wakati viwango vinavyokubalika kimatibabu ni chini ya wiki mbili,” alisema. 
Aliishauri Serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la vifaa katika taasisi hiyo.


Mipango Miji

Alisema ripoti yake imethibitisha halmashauri 148 ambazo ni asilimia 80 zinaendelezwa bila kuwa na mipango kabambe inayoweza kutoa miongozo wa shughuli zote za uendelezaji wa miji nchini. 
“Halmashauri 96 au asilimia 65 kati ya halmashauri 148, hazijawahi kuandaa mipango kabambe tangu zianzishwe,” alisema.
Alisema maeneo mengi yanaendelezwa bila kufuata mipango kabambe iliyopo.
 

Usambazaji dawa
Alisema kwa mujibu wa ukaguzi, imebainika tathmini ya makadirio ya uhitaji wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya afya haufanyiki kwa uhakika.
 

Alisema hali hiyo inatokana na asilimia 50 ya ripoti zinazohitajika za makisio ya dawa za vifaa tiba muhimu kutoka halmashauri za wilaya kutowasilishwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kama inavyotakiwa.
 
“Imebainika asilimia 54 ya oda zinazopokelewa na MSD kutoka bohari za kanda ni kuanzia muda wa siku 14 kulingana na muongozo wa MSD. 


“Hii imesababisha kutetereka kwa mtaji kushuka kwa zaidi ya asilimia 69 kutoka Sh bilioni 81 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 25 mwaka 2013. 
“Hii imechangiwa na ongezeko la deni la Serikali ambalo limeongezeka zaidi ya mara nne kutoka Sh bilioni 14 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 69 mwaka 2014,” alisema CAG.


Kutokana na hali hiyo, CAG alipendekeza uboreshaji wa upatikanaji wa dawa na vifaa muhimu katika vituo vya huduma ya afya. 
“Ninapendekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na MSD kutathimini hali ya mtaji wa uendeshaji wa mfumo mzima wa makisio na usambazaji wa dawa na vifaa tiba muhimu kwa lengo la kutatua tatizo la uhaba wa dawa,” alisema.


Wastaafu,watumishi
Kuhusu wastaafu, ripoti yake imegundua Sh milioni 5.43 zimelipwa kama posho na pango kwa watumishi walioko ubalozini nje ya nchi. 
“Hii ni kinyume na kanuni za kudumu za utumishi, fedha hizo zinazoendelea kulipwa kwa wastaafu hao ambao hawafanyi kazi si zingeweza kulipwa kwa wafanyakazi?” alihoji Profesa Assad.


Majengo ya Serikali
Alisema ukaguzi huo umebaini majengo mengi yanayomilikiwa na Wakala wa Majengo yalijengwa kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita, hali inayosababisha majengo hayo kuwa katika hali isiyoridhisha. 
“Ilibainika hakuna utaratibu madhubuti wa usimamizi wa ukarabati wa majengo ya Serikali, hii ni kwa kuwa mikoa mingi haifuati taratibu zilizopo za ukarabati wa majengo ya Serikali.


“Kati ya mikoa sita iliyotembelewa hakukuwa na mkoa hata mmoja ulioweza kufanya marekebisho ya viwango vilivyowekwa vya ukarabati wa majengo ya Serikali.


“Pia hakukuwa na nyaraka kama vile vitabu vya rejista vya kuweka kumbukumbu ya hali ya ukarabati wa majengo katika ofisi zao na pale ukarabati unapotekelezwa, hutekelezwa bila kuwa na mpango kazi uliowekwa,” alisema.


CAG alipendekeza Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Majengo kuweka sera ya ukarabati wa majengo yanayomilikiwa na Serikali na kufuatilia utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi ya majengo hyo.


Mifumo ya uhifadhi
Alisema katika ukaguzi uliofanyika ilibainika mipango ya usimamizi wa mazingira iliyoandaliwa na Baraza la Usimamizi waMazingira (NEMC), haitilii mkazo suala la viashiria hatarishi.


“Ilibainika NEMC halikutoa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwa makampuni mbalimbali ya migodi inapokiuka sheria hiyo. 
“Na hata pale adhabu zinapotolewa hakukuwa na ufuatiliaji mzuri kuweza kubaini kama adhabu husika imetekelezwa ipasavyo,” alisema.


Alisema pia halmashauri hazifanyi ufuatiliaji wa shughuli katika migodi hali inayosababisha NEMC kushindwa kuwa na picha halisi juu ya utunzaji mazingira katika migodi nchini. 
“Vilevile imebainika kuwa hakuna utaratibu wa shughuli za usimamizi wa mazingira migodini, NEMC ilishindwa kuratibu kwa ufanisi ushirikiano wa wadau mbalimbali katika usimamizi wa mazingira migodini,” alisema.


CAG amependekeza NEMC kutathmini utekelezaji wa mfumo ulipo pamoja na kuanzisha uandaaji wa taarifa itakayoonyesha hali ya mazingira katika sekta madini na kutoa adhabu stahiki kuzuia uvunjaji wa sheria kutojirudia.


Huduma za ugani
Alisema katika uchunguzi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika hawajasambaza kwa ukamilifu miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma za ugani kwa maofisa ugani.


“Pia hakuna vitabu vya rejista na ratiba zinazoonyesha utendaji kazi wa maofisa ugani hali inayosababisha utekelezaji usioridhisha wa mipango na miradi ya mendeleo ya kilimo,” alisema. 
Alisema ripoti hiyo pia ilibaini kuwapo teknolojia duni za shughuli za ilimo, ucheleweshaji wa fedha na kusababisha huduma duni za ugani na ufuatiliaji na tathimini za utoaji wa huduma za ugani kutofanyika ipasavyo.


“Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika zifanye tathmini ya huduma ya ugani na kuangalia na jinsi gani hizo zinaweza kuboreshwa katika maeneo ya uandaaji wa mipango, uratibu, uwezeshaji, ufuatiliaji na utoaji wa mrejesho ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo,” alisema. 


Kauli ya PAC
Akizungumzia ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau alisema inaonyesha mapato ya serikali bado yanapotea na kulitaka Bunge lijalo lipambane na hali hiyo.


“Kwa ujumla hali ni mbaya, kwa mfano Wizara ya Ujenzi ililidanganya Bunge lililopita, angalia Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania), wanaongoza kwa madeni. Lakini pia Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kimetumia fedha vibaya na hili lazima tulishughulikie haraka” alisema Mwidau.

Sinema za Kibongo, bongo movie
Pichani msanii wa sinema za Kibongo Wolper
Mshtuko! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibua maswali kwa mashuhuda walimuona ‘live’ akiingia kwenye hekalu la watu wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemasons yenye nguvu duniani inayohusishwa na imani za kishetani.

TUJIUNGE MTAA WA SOKOINE
Tukio hilo lililoibua kizaazaa kwa mashuhuda waliomuona Wolper, lilijiri juzikati, mishale ya jioni kwenye hekalu hilo lililopo Mtaa wa Sokoine mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

SIMU ZAMIMINIKA
Likiwa kwenye majukumu ya kusaka habari kama kawaida yake, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa mashuhuda hao wakiwataka wanahabari wetu kuwahi eneo la tukio.
Kufuatia umbali waliokuwa mapaparazi wetu, ilibidi kuwaomba mashuhuda hao ‘kumfotoa’ picha ambapo mmoja wao alifanya hivyo na kuziwasilisha kwenye meza ya gazeti hili.

ALINASWAJE?
Akidadavua mazingira aliyonaswa Wolper, shuhuda huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza mwanzoni hatukumjua kama ni Wolper lakini kuna dada ambaye anamjua vizuri na ni shabiki wake mkubwa ndiye aliyetuhakikishia kuwa ni Jacqueline (Wolper).

“Kuna waliomuona akiingia. Nilipofika mimi nilimkuta getini anatoka. Walisema hakukaa muda mrefu kwani alitumia dakika kadhaa kisha akatoka na kwenda kwenye gari lake aina ya Prado (Toyota) alilopaki mbali kidogo na lango hilo,” alisema shuhuda huyo kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:
“Baada ya hapo alitoka nduki maana nzi (watu) walikuwa wameanza kumjalia na kulizingira gari lake.”

WOLPER AJITETEA
Baada ya kuzikagua picha za Wolper akiwa katika mazingira hayo na kujiridhisha kuwa ni yeye, gazeti hili lilimbana mwigizaji huyo ambapo alijitetea:

“Jamani nilikuwa sina hili wala lile. Kuna jengo nilikuwa nalitafuta ndiyo nikajikuta nimetokea maeneo hayo.
“Mimi mwenyewe nilishtuka kuona watu wananiangalia sana kumbe ndiyo nikagundua nipo kwenye lango la Freemasons.”
Risasi Jumamosi: Mbona kuna mashuhuda walikuona wakati unaingia na wakati unatoka?
Wolper: Unajua mimi sikuona kibao chao lakini sikuingia kabisa hadi kule ndani.

Risasi Jumamosi: Lakini kuna madai kwamba wewe ni mwanachama. Unasemaje?
Wolper: Mimi siyo Freemasons, nakumbuka kuna siku watu walinifuata wakaniambia nijiunge Freemasons nitakuwa na mafanikio lakini sijakubaliana nao.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2012 wakati wa kifo cha aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ kuliibuka madai ya baadhi ya wasanii ambao ilisemekana ni ‘memba’ wa Freemasons

Mbali na Kanumba, wengine waliotajwa kwenye listi hiyo mwaka huo alikuwepo Wolper na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye madai hayo yamekuwa yakiendelea kumganda huku wengi wakiwa na imani potofu kuwa ukijiunga na jamii hiyo unapata utajiri wa ghafla.

Source:GPL

Dangote kutengeneza Bandari Mtwara
Alhaji Dangote akisikiliza maelezo ya eneo husika

Mtwara

Wakazi wa kijiji cha Mgao, kata Naumbu katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wametoa hekari 2,500 kwa mwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahaman Shah alimweleza bilionea huyo namba moja Afrika kuwa, wakazi wa kijiji chake wameridhia kumpatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari na kwamba ni imani yao mradi huo utatekelezwa haraka iwezekanavyo.
dangote in tanzania
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Abrahaman Shah akitoa maeleketo

“Sisi wakazi wa Mgao tumekupatia eneo la hekari 2,500 la nchi kavu na bahari ili ujenge bandari, pia tunawapatia ukazi wa kudumu katika kijiji chetu, wewe, balozi na balozi mdogo wa Nigeria hapa nchini, wote ninyi kuanzia sasa ni wakazi wa kijiji cha Mgao,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza; “Kijiji chetu kina wakazi 2026, Alhaji Dangote atakuwa mkazi wa 2029, Balozi Isihaka Majabu atakuwa mkazi wa 2027 na balozi mdogo Salisu Umaru atakuwa mkazi wa 2028…hawa ni wakazi wenzetu wa kijiji cha Mgao,” alisema.

Picha za Dangote akiwa Mtwara


Alhaji Dangote akiwasili
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendegu,
akiwa na mwakilishi wa Dangote, Esther Baruti
Msafara
Msafara
dangote in tanzania
Alhaji Dangote akizungumza na wahandishi wa habari
dangote in tanzania
Ndege iliyomleta ikiondoka

shinyanga
Basi jingine lapata ajali
Habari zilizotufikia ni kuwa basi lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora liligongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga. 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa alibainisha kuwa, watu 10  wamepoteza maisha huku 51, wakijeruhiwa vibaya na kuendelea kukimbizwa hospitali.

ajali shinyanga

Basi lagongana na Lori na kuua

“Hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha. Na tunaendelea kuokoa wengine ambao 51 ni majeruhi. hivyo bado tupo hapa kwa sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa”
Hadi sasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.



Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amen, na Mwenyezi Mungu awajaalie nafuu ya haraka majeruhi wote.

mwananchi, Nyrere Foundation
Joseph Butiku, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalim Nyerere
“Mchakato huu una mambo makuu mawili ya kuamua ambayo ni kura ya Ndiyo au Hapana. Hivyo basi kupiga kura ya Hapana siyo dhambi kwani inatoa nafasi kwetu sote kukaa tena na kuangalia upungufu uliojitokeza na kilichosababisha upungufu huo nini ili tusirudie tena makosa,” alisema Butiku na kuongeza:

“Kura ya ndiyo inamaanisha tunaikubali Katiba Inayopendekezwa, hata ikiwa haina mashiko itaendelea kutumika kwa vile mmeikubali, lakini nisisitize kwamba kura ya hapana siyo dhambi, ipo kisheria na asije mtu akawaambia mpigie kura ya ndiyo.


Alisema kabla ya kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa ni vyema ikashindaniwa kwa hoja na si kwa nguvu au ngumi huku akiwataka vijana nchini kutothubutu kujiingiza kwenye mikumbo inayoweza kusababisha nchi ikaingia kwenye machafuko.

Aliyasema hayo kwenye mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na taasisi hiyo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku) jijini Mbeya, Butiku alisema kura ya Hapana au Ndiyo, zote zinatoa fursa sawa kwa wananchi kuamua kwa utashi wao.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mbeya, Butiku aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, alieleza kuwashangaa viongozi wa vyama na Serikali kuwachagulia wananchi kura ya Ndiyo.

Akitolea mfano wa chama chake cha CCM, Butiku alisema hakitakiwi kuwahadaa Watanzania na kuwataka kuipigia kura ya Ndiyo katiba hiyo, badala yake kiwaache waamue wenyewe.
Aliwataka wananchi watumie muda huu kuitafuta nakala ya Katiba Inayopendekezwa, waisome na kuielewa ili hatimaye waamue ama kuipigia kura ya Hapana au Ndiyo.

WANANCHI WAVAMIA SHAMBA LA MWEKEZAJI

Yafuatayo ni baaadhi ya mabango yaliyokutwa katika Karamu Estate lililopo kijiji cha Nndatu wilayani Arumeru, Arusha baada ya wananchi kuvamia shamaba hilo usiku wa manane na kuamua kuotesha migomba.







ONA MAONI GANI KUHUSU HILI?

Wananchi wakiboboa Nguzo katika mtaa wa Makoroboi, Mwanza


Wananchi wa Mkoa wa Mwanza, jana waliungana kuboboa ujenzi uliojengwa katika njia ya Mtaa wa Makoboi.

Mabomu yarindima Mwanza, katika ugomvi wa wamachinga na Wahindi

Mwandishi wetu akizungumza na mmoja ya mwananchi alisema, “Hii njia ipo tangu enzi za mjerumani na Mjerumani alikua akipita hapa na kwenda pale juu mlimani, haiwezekani hawa wahindi waje wanunue njia hii. Nyerere asingeruhusu haya yatokee”
Wengine walisikika wakisema “Peoples……Power"

Ujenzi huu wote inaaminika umekua ukifanyika usiku kwa usiku

Nguzo zilizowekwa
Baada ya kuboboa nguzo
Wananchi wa boboa nguzo katika mtaa wa Makoroboi, Mwanza

Ukuta uliojengwa katika Mtaa wa Makoroboi, Mwanza
USISITE KUTOA MAONI YAKO KUHUSU HILI TUKIO AMBALO NI ENDELEVU
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE