Joseph Butiku,Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere |
Joseph Butiku,Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere amesema
nchi inaongozwa na Katiba, lakini inashangaza viongozi wa chama chake cha CCM
na vingine ndiyo wanaongoza kwa kuvunja sheria na taratibu.
“Huko nyuma kulikuwa na matatizo, lakini sasa chama changu (CCM)
na vyama vingine ndiyo magwiji wa kuvunja taratibu,” alisema Butiku wakati
akichangia hoja jana kwenye mdahalo wa umuhimu wa Kulinda Amani na Umoja
uliorushwa moja kwa moja na ITV.
“Mtandao huo iliamua kufanya kazi nje ya CCM kwa
sababu itikadi zao na sisi zilitofautiana. Eti wanasema CCM ni chama cha
mizengwe kinawachelewesha kutajirika. Sasa hao watu ndiyo wameendelea kuwapo na
kusababisha haya matatizo yaendelee,” alisema Butiku.
“Kama baadhi wa watu muhimu wapo nje, sasa
mwenyekiti wetu (Rais Jakaya Kikwete) amekwenda kufanya nini huko? Kama
viongozi wa CCM wameshampata mtu wanayemtaka (kugombea urais) wanakwenda Dodoma
kufanya nini. Huku si kumkejeli Rais Kikwete?” alihoji.
Alisema viongozi hawafuati utaratibu, kila kitu
lazima hela. “Sasa tunatoka kwenye utaratibu wetu wa vyama tunashiriki katika
kufanya uovu. Kama haki inauzwa, hatuwezi kupata amani. Viongozi wanatoa rushwa
hata kabla ya kupewa nchi. Je, wakipewa nchi itakuwaje?” alihoji.
Tweet