Joseph Butiku, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalim Nyerere |
“Mchakato huu una mambo makuu mawili ya kuamua ambayo ni kura ya
Ndiyo au Hapana. Hivyo basi kupiga kura ya Hapana siyo dhambi kwani inatoa
nafasi kwetu sote kukaa tena na kuangalia upungufu uliojitokeza na
kilichosababisha upungufu huo nini ili tusirudie tena makosa,” alisema Butiku
na kuongeza:
“Kura ya ndiyo inamaanisha tunaikubali Katiba Inayopendekezwa,
hata ikiwa haina mashiko itaendelea kutumika kwa vile mmeikubali, lakini
nisisitize kwamba kura ya hapana siyo dhambi, ipo kisheria na asije mtu
akawaambia mpigie kura ya ndiyo.
Alisema kabla ya kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa ni
vyema ikashindaniwa kwa hoja na si kwa nguvu au ngumi huku akiwataka vijana
nchini kutothubutu kujiingiza kwenye mikumbo inayoweza kusababisha nchi
ikaingia kwenye machafuko.
Aliyasema hayo kwenye mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na taasisi
hiyo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku) jijini
Mbeya, Butiku alisema kura ya Hapana au Ndiyo, zote zinatoa fursa sawa kwa
wananchi kuamua kwa utashi wao.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mbeya,
Butiku aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji
Joseph Warioba, alieleza kuwashangaa viongozi wa vyama na Serikali kuwachagulia
wananchi kura ya Ndiyo.
Akitolea mfano wa chama chake cha CCM, Butiku alisema hakitakiwi
kuwahadaa Watanzania na kuwataka kuipigia kura ya Ndiyo katiba hiyo, badala
yake kiwaache waamue wenyewe.
Aliwataka wananchi watumie muda huu kuitafuta nakala ya Katiba
Inayopendekezwa, waisome na kuielewa ili hatimaye waamue ama kuipigia kura ya
Hapana au Ndiyo.
Tweet