|
Alhaji Dangote akisikiliza maelezo ya eneo husika |
Mtwara
Wakazi wa kijiji cha Mgao, kata Naumbu katika
halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wametoa hekari 2,500 kwa mwekezaji wa kiwanda
cha saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ili ajenge bandari itakayotumika
kusafirisha saruji kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na
nje ya nchi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahaman Shah alimweleza bilionea
huyo namba moja Afrika kuwa, wakazi wa kijiji chake wameridhia kumpatia eneo
kwa ajili ya ujenzi wa bandari na kwamba ni imani yao mradi huo utatekelezwa
haraka iwezekanavyo.
|
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Abrahaman Shah akitoa maeleketo |
“Sisi wakazi wa Mgao tumekupatia eneo la hekari 2,500 la nchi kavu
na bahari ili ujenge bandari, pia tunawapatia ukazi wa kudumu katika kijiji chetu,
wewe, balozi na balozi mdogo wa Nigeria hapa nchini, wote ninyi kuanzia sasa ni
wakazi wa kijiji cha Mgao,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza; “Kijiji chetu
kina wakazi 2026, Alhaji Dangote atakuwa mkazi wa 2029, Balozi Isihaka Majabu
atakuwa mkazi wa 2027 na balozi mdogo Salisu Umaru atakuwa mkazi wa 2028…hawa
ni wakazi wenzetu wa kijiji cha Mgao,” alisema.
Picha za Dangote akiwa Mtwara
|
Alhaji Dangote akiwasili |
|
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendegu,
akiwa na mwakilishi wa Dangote, Esther Baruti |
|
Msafara |
|
Msafara |
|
Alhaji Dangote akizungumza na wahandishi wa habari |
|
Ndege iliyomleta ikiondoka |