WATOTO 17 WAFICHWA NA KUPATIWA MAFUNZO YA KIISLAM KWA SIRI
Watoto wa Kiislam |
Umati
mkubwa wa wakazi wa mji wa Moshi wamejitokeza katika kata ya Pasua mjini Moshi
kushuhudia tukio la watoto hao wenye umri wa kuanzia miaka miwili
hadi 13 ambao walikuwa wanaishi kwa Bw.Abdelnasir Abrahamani ambaye ni
mfanyabiashara wa nguo nchini Kenya.
Akizungumza
katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Moshi Bw.Novatus Makunga amesema tatizo
hilo kwa mji wa Moshi ni kubwa na kwamba kwa sasa nyumba hiyo imefungwa na
kuondolewa watoto hao ili warejeshwe kwa wazazi hao wakati hatua za kisheria
zikiendelea.
Mmoja
wa wazazi mwenye watoto watatu waliopotea tangu mwezi February mwaka jana na
kukutwa katika nyumba hiyo Bw.Ramadhani Mohamedi amesema aligundua tukio hilo
baada ya kukutana na mtoto wake wa kike barabarani na kumweleza mateso
wanayoyapata huko.
Naye
mfanyabiashara huyo Bw.Abdulinasir Abrahamani amesema nyumba hiyo ni familia na
ndugu zao wa kiislamu lakini siyo kituo cha yatima, ila ni sehemu ya kutolea
mafundisho ya dini ya kiislamu.
Tweet