Baadhi ya Watoto 18 |
Taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela imeeleza
kuwa hayo yalibainika katika mahojiano baina ya watoto na askari wa dawati la
jinsia.
Alisema
watoto hao wanatoka mikoa mbalimbali ikiwamo Tanga, Mara, Kagera, Mbeya na
Dodoma.
Kamanda
Kamwela alisema pia wamegundua kuwa watoto walikuwa wakiishi kwenye mazingira
magumu ikiwamo kulala chini katika chumba kidogo.
Alisema
polisi linawashikilia watu wawili (mume na mke) ambao wanatuhumiwa kuwahifadhi
watoto hao.
Kamanda
huyo alisema watoto hao wana umri wa kwenda shule, lakini walikuwa hawasomi.
Alisema
polisi wanachunguza aina ya masomo ya dini waliyokuwa wakifundishwa.
“Lazima
tuchunguze uhalali wa masomo ya dini waliyokuwa wakisoma ili tujue kama kweli
watoto hawa walipelekwa na wazazi wao au la, kwa kuwa watoto hao walipaswa kuwa
shuleni” alisema Kamanda Kamwela.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga alisema watoto hao walikuwa wakiishi kwenye
mazingira magumu, huku wakipewa adhabu kali ikiwamo kubeba matofali mgongoni
pindi wanapokosea.
“Maelezo
ya watoto yanaonyesha walikuwa wakiteswa, adhabu hizi kwa watoto ni kubwa, bado
tunawachunguza ili tujue kila kitu na walichukuliwaje huko majumbani kwao,”
alisema Makunga.
Alisema
kwa wazazi watakaowatambua watoto wao, wanapaswa kwenda na uthibitisho ikiwamo
cheti cha kuzaliwa au uthibitisho mwingine utakaoonyesha ni mzazi halisi.
Tweet