Tukio
hilo lilitokea saa 8:00 usiku, majambazi hayo yalifunga Barabara ya
Mwanza-Musoma kwa muda na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Kisesa huku milio
ya bunduki ikitawala anga.
Wakizungumza
na Habari Duniani eneo la tukio jana, mashuhuda walisema walianza kusikia milio
mizito ya vitu kama bomu na kwamba baada ya muda wakaona watu wakivamia duka la
mfanyabiashara huyo na kupiga risasi hewani.
Mmoja
ya mashuhuda hao, alisema “Mimi ni fundi baiskeli hapa stendi jana (juzi) muda
kama wa saa mbili usiku nilisikia sauti ya vishindo kama bomu, lakini baada ya
muda nikasikia sauti za bunduki hewani,”
Aliongeza:
“Kwa kweli tulitawanyika watu wote hapa mtaani na kuacha mali zetu. Baada ya
kutulia tulikuja kushuhudia nini kilitokea, lakini tulikuta mtu mmoja ambaye ni
mfanyabiashara hapa Kisesa anavuja damu tulimuangalia tukamkuta amefariki.”
Shuhuda
mwingine, alisema watu hao walifunga Barabara ya Mwanza-Musoma na kwamba,
walikuwa wakipiga risasi ovyo hewani.
Aliendelea
kusema hali ilikuwa mbaya, kwani hawakuwahi kushuhudia tukio kama hilo na mtu
aliyefariki alikuwa mfanyabiashara maarufu Kisesa.
Mwandishi
wa habari hizi jana alifika Kituo cha Polisi Kisesa ambako askari wa kituo
hicho walikiri kuwapo kwa tukio hilo huku wakitaka atafutwe Kamanda wa Polisi
wa Wilaya ya Magu.
Kamanda
wa Polisi Magu, Charles Mkapa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini
akadai msemaji mkuu ni Kamanda wa Polisi Mwanza.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Robert Mnyandwa alimtaja mfanyabiashara
aliyefariki baada ya kupigwa risasi na majambazi hao kuwa ni Nestory Andrew
mkazi wa Igoma.
Mnyandwa
alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba, hata
thamani ya mali na fedha zilizoporwa haijajulikana kwani mhusika alifariki
dunia.
“Ni
kweli tukio limetokea jana saa mbili usiku na mtu mmoja ambaye ni
mfanyabiashara wa Kisesa alipigwa risasi na kupoteza maisha. Bado hatujamkamata
mtu na tunaendelea na uchunguzi,” alisema Mnyandwa.
Kufungwa
kwa mitaa na majambazi, kumesababisha wafanyabiashara hasa wanaojihusisha na
biashara ya fedha kwa mitandao kufunga maduka yao mapema.
Wafanyabiashara
kadhaa wamekwishauawa ama kuporwa fedha zao kutokana na majambazi hayo kuvamia
maduka yao.
Tweet