UTANGULIZI

Tarehe 22 Januari, 2015 kuanzia saa tano hadi sita mchana, Wizara inatarajia kuongea na waandishi wa habari ili kuufahamisha umma wa Watanzania kuhusu fursa za ajira katika Shirika la Ndege la Emirates kuanzia mwaka 2015. Katika tukio hilo ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo kunatazamiwa na kuwepo na uwakilishi kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) pamoja na mwakilishi wa Shirika la Ndege la Emirates kwa Tanzania.

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
Katika kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya nchi, Wizara kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania ulioko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umefanikiwa kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka huu 2015.

Shirika hilo la Ndege limekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali ambapo maafisa wake wanaosimamia ajira watakuja Tanzania mwezi Machi 2015 kwa ajili ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi wa awali.

Shirika la Emirates litaajiri kada mbalimbali kuanzia Maintenance Technicians/Mechanics, Planners-Ground Handling, Metal Workers, Customer Service Professionals na Cabin Crews.

Lengo kuu la kuongea na Waandishi wa Habari ni kuutangazia Umma wa Watanzania kuchangamkia ajira hizo ambazo awali zilitangazwa mwezi Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu waliomba wakati huo na hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa. Baada ya mazunguzo ya kina, Uongozi wa Shirika la Ndege hilo umekubali kuongeza muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine, na kupanga kufanya usaili kama ilivyoelezwa hapo awali.

Serikali kwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikishirikiana na Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Ajira inawatangazia Watanzania wote wenye sifa na vigezo vinavyotakiwa wachangamkie fursa hizi za ajira bila kukosa.

Waombaji wanaweza kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia anuani yaemirates.com/careers. Aidha, waombaji wanashauriwa kuuarifu Ubalozi Mdogo kwa barua pepe (tzconsdb@emirates.net.ae) mara baada ya kuwasilisha maombi yao ili kurahisisha ufuatiliaji. Mwisho wa kuwasilisha maomba ni tarehe 15 Machi, 2015, wakati usaili umepangwa kufanyika tarehe 29 Machi, 2015.

HITIMISHO
Watanzania wote mnahimizwa kutumia fursa hii adhimu kuomba nafasi hizi kwa wale wenye sifa na vigezo stahiki, na pia kujiandaa vema katika usaili ili Tanzania iweze kufanya vizuri kama wenzetu wengine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ambao kwa sasa wameajiriwa kwa wingi sana katika soko la Ajira la UAE.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
  • 90 years old woman found in school studying.
    Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita…
  • MAYWEATHER ATUA DAR ES SALAAM
    Floyd Mayweather Bondia maarufu duniani kwa sasa Floyd Mayweather baada ya kumpiga Emmanuel "Manny"…
  • 32 DEAD, 80 WOUNDS IN YOLA, NIGERIA EXPLOSION
    Yola, Nigeria. An explosion occurred in the city of Yola, Nigeria. The night-time blasts ripped through…
  • WATOTO WAFICHWA NA KUPATIWA MAFUNZO YA KIISLAM KWA SIRI
  • MAGAZETI YA LEO
    Kama kawaida Habari Duniani inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia…
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014 - TANZANIA CSEE 2014 RESULT
    MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014 BOFY HAPA CSEE 2014 RESULT CLICK HERE
  • KATIBA INAYOPENDEKEZWA IMEFUTA MAMBO MUHIMU 70 - POLEPOLE ACHAMBUA
  • Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao
    Pambano la masumbwi linalosubiriwa na ulimwengu mzima kati ya mabondia wawili bora katika miaka ya hivi…
  • WAZIRI ASHINDWA UCHAGUZI NA KUMSHAMBULIA MSIMAMIZI
    Dk Titus Kamani ashindwa uchaguzi Hali ilikuwa mbaya jimboni Busega ambako baada ya Dk Kamani na wafuasi…
  • Why, Your Supposed to do this Business? Celebrities and Ordinary people
    This is the business fit everyone either you are celebrity or ordinary person. Celebrities refers to…

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE