Mechi hiyo ilifanyika Katika
uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huku Nigeria wakipata nafasi ya ku-tosi
na kupata mikimbio 105
Wenyeji walifanikiwa kupata
mikimbio 108 na kupoteza wiketi 7 katika zamu yao huku Salum Jumbe akipata
mikimbio 45 katika mipira 64 aliyopiga. Kwa upande wa Nigeria, Akachukwu Chima
alifanikiwa kupata mikimbio 22 katika mipira 50 aliyopiga.
Matumaini ya wenyeji Tanzania
kufuzu yaliingia doa baada ya kufungwa kwa Kenya kwa runs 11 katika mechi nzuri
ya kuvutia ya kufuzu iliyochezwa katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya pili
kwa wenyeji kupoteza, hivyo kutoa nafasi kwa Namibia, iliyoshinda mechi zote
nne, baada ya kuwafunga Uganda kwa runs 39 katika mechi iliyofanyika Gymkhana
Club.
Botswana pia iliwafunga Kenya
kwa mikimbio 10 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Annadil Burhani.
Michuano hiyo inaisha Alhamis
na Namibia ikiwa na pointi 8 baada ya kushinda mechi zote, ikiwa katika nafasi
nzuri ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia, kutegemea na matokeo ya mechi za leo.Wenyeji Tanzania , Kenya na Uganda (zote zikiwa na pointi 4 kila moja) pia zina nafasi ya kufuzu na kugombania nafasi ya pili ili kucheza katika michuano ya mwisho ya kufuzu itakayofanyika Bangladesh kwa ajili ya kutafuta tiketi ya mwisho, endapo Namibia itafuzu..
Nigeria na Botswana zina
nafasi finyu baada ya kila moja kuwa na pointi 2 katika michezo mine iliyocheza
(kila moja).
Tweet