Daktari
wa usapuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha kwamba mwanamme wa kwanza
aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.
Professor Andre van der Merwe,
ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba, ameiambia BBC kwamba mwenza
wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.
Mwanamme huyo mwenye umri wa
miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anapashwa tohara ambayo haikufanikiwa.
Professor van der Merwe
ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo wa kiungo
umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku zijazo.
Tweet