Albert Woodfox sasa yuko huru baada ya kuzuiliwa upweke miaka 40 jela |
Jaji
mmoja katika jimbo la Louisiana nchini Marekani ameamuru kuachiliwa huru kwa
mfungwa ambaye amekuwa akizuiliwa bila kupewa ruhusa ya kutangamana na watu
wengine kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40. Jaji James Brady kadhalika amewapiga
marufuku viongozi wa mashtaka kumfungulia tena mashtaka kwa mara ya tatu Albert
Woodfox, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 68.
Amekuwa kizuizini bila
kuruhusiwa kuonana na mtu yeyote tangu tarehe 18 mwezi Aprili mwaka 1972
kufuatia vurugu za gerezani ambazo zilisababisha kifo cha askari jela mmoja.
Woodfox alifunguliwa mashtaka
na kesi yake kusikilizwa mara mbili lakini mashtaka yote mawili yalitupiliwa
mbali baadaye. Anazidi kukanusha mashtaka hayo.
Siku ya jumatatu, Jaji Brady
aliamuru Woodfox kuachiliwa huru bila masharti yoyote, na vilevile kuwazuia
viongozi wa mashtaka kumfungulia mashtaka menginne akisema haitakuwa haki.
Angola Three
Woodfox ni mwanachama wa
mwisho wa kundi la wafungwa watatu wanaojulikana kama ''Angola Three''
Read more at BBC Swahili
Tweet