NESI, HOSPITALI
MANESI WAKISHIRIKISHANA JAMBO
Muuguzi aliyekuwa zamu katika kituo cha Afya cha Muungano wilayani Chamwino, Dodoma aliamua kumchapa viboko mjamzito huyo baada ya kumuona anashindwa kujikakamua ili kumsukuma mtoto atoke na alikuwa akifanya hayo akidai kuwa mwanamke huyo ni mzembe na anadeka ndio maana alikuwa anashindwa kujifungua.

Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikiri kuwapo kwa taarifa za mama huyo kuchapwa viboko akiwa chumba cha kujifungulia na kwamba wameagiza uchunguzi ufanyike ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo na hatua zichukuliwe.

Muuguzi huyo ni mmoja tu kati ya wengi ambao wamekuwa wakiwafanyia vitendo visivyo sahihi wagonjwa wanapoenda hospitalini kwa ajili ya kupata tiba, hasa wajawazito ambao hulundikiwa mzigo wa maneno kuanzia wanapofika hadi wanapojifungua. Imekuwa ni kawaida kwa kina mama wajawazito kusimangwa, kutolewa maneno machafu na kucheleweshewa huduma na matokeo yake baadhi hujikuta wakipoteza watoto na wengine kulazimika kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji.

Wakati mama huyo akiendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, ni vizuri kwa uongozi wa mkoa kufanya uchunguzi wa kina kama ulivyoahidi ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo lililotokea Aprili 3 mwaka huu, takriban siku 20 zilizopita.

Imekuwa ni kawaida kwamba tukio lolote baya likiripotiwa na vyombo vya habari, wahusika huwa wepesi kusema wanafuatilia kupata taarifa kamili na wanapoona hali imepoa, nao wanachana nalo na hakuna hatua zinazochukuliwa. Matokeo yake ni vitendo hivyo kuendelea kuwa sugu.

Itakuwa ni kitu cha ajabu kama Serikali inapiga kelele kuhimiza wananchi kwenda kwenye vituo vya afya au hospitalini wakati wauguzi nao wanafanya vitendo ambavyo vinakatisha tamaa wananchi kwenda sehemu hizo.

Toa maoni yako juu ya huyu nesi na serikari. Kama unatumia facebook, twitter, google + au jiandikishe na utoe maoni yako. Karibuni.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
  • 4 U MOVEMENT (TEAM LOWASSA) WAJIUNGA CHADEMA
    Vijana wanao aminika kua ni wafuasi wa Lowassa wahamia CHADEMA.
  • HAVE YOU READ TODAY UK FRONT PAGES NEWSPAPER? READ NOW
    HabaruDuniani brings to you UK front pages Newspaper at your finger tips. Please do not forget to like our…
  • * WABUNGE WAPYA WA UKAWA (CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI)
    MAJIMBO MAPYA YA UKAWA (CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI) James Mbatia ashinda Ubunge…
  • MAGUFULI SACK TANZANIA ANTI-CORRUPTION BODY CHIEF DR.HOSEAH
    Tanzania President Dr. Magufuli sacks Director General of The Prevention and Combating of Corruption…
  • ARUMERU: WANANCHI WAVAMIA SHAMBA LA MWEKEZAJI LA KARATU ESTATE
    WANANCHI WAVAMIA SHAMBA LA MWEKEZAJI Yafuatayo ni baaadhi ya mabango yaliyokutwa katika Karamu Estate…
  • WALIOWAJERUHI POLISI TANZANIA TANGA WANASAKWA
    Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani…
  • First vehicles manufactured in Uganda and Kenya - Kiira and Mobius
    This is a car developed in Uganda by Kiira Motors Corporation (KMC), origionally…
  • 2ND MINERAL SANDS REPORT:LIST OF MANY TO BE INTERROGATED
    Dar es Salaaam. Speaking at the State House yesterday after receiving a report from an eight-member team led…
  • 3 WAYS TO AVOID WHATSAPP FEE OR TRIAL PERIOD
    Are you the power user of WhatsApp? Before getting started, let me clear that we all know and use…
  • 999TSH MIL TO FREE EDUCATION IN MWANZA SCHOOLS - GOVT
    Mwanza. The Treasury has disbursed Tsh.999 million to finance free education in both primary and secondary…

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE