Mohammed Dewji |
TAJIRI KIJANA KULIKO WOTE AFRIKA
Mohammed
Dewji has seen his net worth rise considerably over the past year as his MeTL
group, a conglomerate in 11 countries with interests in trade, FMCG and
manufacturing, undergoes significant expansion.
Jarida la Forbes la Marekani
limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na
utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara
mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl
Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa
na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea
huyo Mtanzania .
“Alinunua viwanda vya nguo na
mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na
faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti
hiyo.
Metl ina viwanda vya
kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula,
sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani
(Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.
Katika kampuni hiyo, ambayo
imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa,
Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.
Kwa mujibu wa tovuti yake,
Metl inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda
nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati
na petroli na utengenezaji baiskeli.
Pia inahusika na huduma za
simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es
Salaam.
Dewji anashika nafasi mbili
juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz
Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho.
Rostam amefungana nafasi ya 26
na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na Femi Otedola wenye utajiri wa
Sh1.8 trilioni kila mmoja.
Orodha hiyo ya 29 bora
inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa na utajiri wa Dola 15.7
bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango ambacho ni mara moja na nusu ya
bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka 2014/15.
Forbes linamtaja Rostam kuwa
na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.8 trilioni),
kiwango ambacho kimebaki pasi na mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana. Rostam
anamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya
Vodacom.
Tweet