Mvua ya Mawe |
Watu wasiopungua 30 wamepoteza maisha na wengine wasiopungu 80 kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali
kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo
ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500 bila makazi katika
kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya mifugo ikisombwa.
Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata ya Mwakata
kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Maafisa
wa polisi wanasema kuwa mvua kubwa na upepo mkali ziliharibu nyumba na kufunga
barabara karibu na mji wa Shinyanga na hivyobasi kuzuia oparesheni za
kuwanusuru watu.
Waandishi wanasema kuwa mimea
imeharibiwa na mifugo kuuawa.
Hali ya
majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa
baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
Habari Duniani tunatoa Pole waathirika woote.
Tweet