Showing posts with label Gwajima. Show all posts
Showing posts with label Gwajima. Show all posts

GWAJIMA
BASTOLA NA RISASI ZA GWAJIMA
Tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.

Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima. Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina  hizo zilizokamatwa.

Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.

Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.


KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
S. H. KOVA,
DAR ES SALAAM.

Prof.Lipumba, CUF,Josephat Gwajima, ufufuo na Uzima
Prof.Lipumba akiwa na Josephat Gwajima

LIPUMBA AMTEMBELEA ASKOFU DR. JOSEPHAT GWAJIMA

Profesa Ibrahim Lipumba,mchana wa Leo amemtembelea Askofu Josephat Gwajima aliyelazwa TMJ Hospital.

Amefurahi kuona hali yake inazidi kuimarika na ameshatoka kwenye wodi ya wagonjwa mahututi,(ICU).


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE