Vatican.
Baba Mtakatifu Papa Francis ameomba radhi
wakati anaongoza mkutano wa wiki tatu wa baraza la makardinali na maaskofu
kujadili namna ya kupitia mafundisho ya kanisa hilo pamoja na kuhusu masuala ya
familia.
Papa
Francis ameuomba msamaha huo alipokuwa akiwahubiria maelfu ya watu
waliokusanyika kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, mjini Vatican,
katika utaratibu wake wa kila juma.
''Kabla ya kuanza kwa
Katekesi, nataka kwa niaba ya Kanisa, kuomba msamaha kwa kashfa ambazo hivi
karibuni zimeikumba Roma na Vatican. Naomba msamaha wenu,'' alisema Papa
Francis.
Msamaha huo ameuomba katika
kipindi ambacho Kanisa Katoliki limejikuta kwenye kashfa kadhaa, ikiwemo ile ya
kujitokeza hadharani kwa Padri shoga anayepinga msimamo wa kanisa kuhusu
mapenzi ya jinsia moja na kauli dhidi ya Meya wa Roma, aliyejiuzulu wiki
iliyopita.
Hata hivyo,
Papa hakutaja hasa aina ya kashfa anayoizungumzia wala kutoa mifano. Siku moja
kabla ya kuanza kwa mkutano huo kuhusu masuala ya familia, padri wa Poland
alitangaza hadharani kuwa yeye ni shoga, huku mpenzi wake akiwa pembeni yake.
Padri huyo aliyefanya kazi yake Vatican kwa miaka 17, alifukuzwa kazi yake ya
ukasisi.