MAJIMBO MAPYA YA UKAWA (CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI)
James Mbatia ashinda Ubunge Vunjo
James
Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ameibuka mshindi baada ya kumshinda
mwanasiasa mkongwe Augustine Mrema wa Tanzania Labour Party (TLP).
James Mbatia amabye alikua akiwakilisha UKAWA alipata kura 60,187 wakti mpinzani wake wa karibu Innocent Shirima wa CCM alipata kura 16,617 na Augustine Mrema alipata kura 6,416.
Hii ni mara ya pili kwa Mbatia kua Mbunge wa Vunjo. Mara ya kwanza ni 1995 wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.
James Mbatia amabye alikua akiwakilisha UKAWA alipata kura 60,187 wakti mpinzani wake wa karibu Innocent Shirima wa CCM alipata kura 16,617 na Augustine Mrema alipata kura 6,416.
Hii ni mara ya pili kwa Mbatia kua Mbunge wa Vunjo. Mara ya kwanza ni 1995 wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.
Wilfred Lwakatare (CHADEMA) ashinda Ubunge Bukoba Mjini
Jimbo
la Bukoba mjini lililokua chini ya CCM chini ya Khamis Kagasheki limechukuliwa
na Wilfred Lwakatare wa CHADEMA. Lwakatare alipata kura 28,112 na Kagasheki
kura 25,565.
Michael Jaffar (CHADEMA) ashinda Ubunge Moshi mjini
Jaffar amemshinda mpinzani wake wa karibu David Mosha wa CCM na
kutangazwa mshindi. Jaffar alipata kura 51,646 wakati Mosha alipata kura 26,920.
Joseph Haule (CHADEMA) ashinda Ubunge Mikumi
Haule
aka Profesa J, ambaye ni mwanamziki amepata kura 32,256 na mpinzani wake wa CCM
Jones Nkya amepata kura 30,425.
Joseph
Haule amekua mwanamziki wa pili kua Mbunge baada ya Joseph Mbilinyi “SUGU”.
Abdallah Mtolea (CUF) ashinda Ubunge Temeke
Abdallah
Mtolea amefanikiwa kumshinda Abbas Mtemvu (CCM). Mtolea amepata kula 103,231
dhidi ya kura 97,555.
Jimbo
la Temeke hii ni mara ya pili kuchukuliwa na upinzani, mwaka 1995-2000
ilichukuliwa na Augustine Mrema alishinda kupitia NCCR-Mageuzi.
Maulid Mtulia (CUF) ameshinda Ubunge jimbo la Kinondoni
Mgombea
ubunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia ametangazwa
mshindi wa nafasi hiyo katika jimbo la Kinondoni, akimshinda mgombea wa CCM,
Idd Azzan.
Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa
uchaguzi katika jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni,
Mussa Natty amesema, Mtulia amepata kura 70, 337 huku Azzan aliyekuwa anatetea
kiti chake akipata 65,964.