Raisi wa Zamani wa Misri, Mohammed Morsi |
Misri.
Makahama nchini Misri imemhukumu aliyekuwa rais wa zamani Mohammed
Morsi kifungo cha miaka 20 jela kutokana na kuuawa kwa waamdamanaji wakati
akiwa madarakani.
Hii nidyo
hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja ya
hukumu zinazomuandama.
Morsi
aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani
ya kupinga uongozi wake.
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa
kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa
upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati
ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini
wakakataa kufanya hivyo.
Muslim Brotherhood
Baadaye
Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye
makabiliano, wengi kutoka kwa Muslim Brotherhood.
Kabla ya
kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta
al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.
Tweet