Bunge la Tanzania |
Bunge
la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa
mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha vipengele muhimu vya
ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo limesisitiza serikali kupitia
taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini uwezo kuhusu ajira wazoomba na
mienendo yao kijamii.
Sheria hiyo pia inawataka
watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana na sifa zao. Huku wageni
wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji ili kuleta ushindani sahihi
katika soko la ajira nchini humo.
Sheria hiyo inalenga kuvutia
waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa
wazawa.Akichangia muswada huo kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse
anaeleza jinsi wazawa wanavyopaswa kunufaika zaidi.
Gaudensia Kabaka ni waziri wa
kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema kuwa vibali vya kazi kwa wageni na
suala la uraia kwa mjibu wa sheria hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali
kinachotakiwa ni kutumiza masharti yote mawili.
Kupitia muswada huu,bunge
limesema kuwa ni moja ya hatua itakayosaidia ajira wa vijana wa Tanzania ambayo
baadhi yao wanakosa ajira kutokana na mazingira ya kipaumbele kuwa kwa wageni
na si wazawa kama ilivyo katika mataifa mengi duniani ambayo kutoa fursa kwa
wenyeji na kisha wageni baadaye.
Tweet