Mahakama
kuu ya Tanzania imepokea msaada wa mashine 38 za kupiga chapa Kutoka Mahakama
ya mauaji ya Kimbari(ICTR) itakayorahisisha upatikanaji wa nakala za hukumu na
mwenendo wa kesi mbalimbali hapa nchini.
Akipokea
Msaada huo Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman alisema kuwa msaada huo
utasaidia upatikanaji wa haki kuwa rahisi pia, kwani umekuja wakati muafaka
wakati mahakama ikiwa katika mabadiliko ya kuzifanya kesi kwenda kwa wakati.
Jaji
Othman alisema changamoto ya utoaji haki kwa wakati imeweza kurahisishwa kwa
upatikanaji wa mashine hizo ambazo ni za kisasa na za gharama ambazo
zimeipunguzia mzigo serikali.
“Mashine
hizi za msaada baada ya kupatikana sasa ni mwendelezo wa mashirikiano
yetu kati ya serikali na mahakama hii ikiwemo ukamataji wa wahalifu, kuwatunza
na kuwalinda hivyo ni moja ya faida za mashirikiano hayo”alisema Jaji Mkuu.
Alisema
kuwa ushirikiano uliopo kati ya mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari na
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wa muda mrefu kuanzia kwenye
ukamataji wa wahalifu wa mauji hadi kuwahifadhi hivyo hii sehemu ya
mashirikiano hayo ya muda mrefu.
Jaji
Othman alisema kuwa Hatua ya msaada huo itaendana vizuri na ufundishaji wa
makatibu wetu ilikuweza kufanyakazi kiufanisi kwa kutumia msaada huo wa
vitendea kazi hivyo akaiomba mahakama hiyo kuendana na mbio za kiutendaji ili
kufanikisha upatikanaji haki kwa wakati.
Mashine
hizo zenye thamani ya dolla 95,000 zimetolewa na mahakama ya mauaji ya Kimbari
kwa mahakama yetu ili ziwezekusaidia kupunguza malalamiko na uchelewaji wa
kutoa nakala za hukumu na mwenendo wa kesi za jinai hapa nchini.
“Vitendeakazi
hivi vimekuja wakati muafaka kwani tumekuwa katika mikakati ya ubadilishaji wa
utumiaji wa kuandikia mikono kwenda kwenye utumiaji wa vifaa kutakakorahisisha
kutoa hukumu na mwenendo wa kesi kwa wakati na kuacha kutumia muda mrefu kupata
nakala za hukumu na mwenendo wa kesi mbalimbali” alisema Jaji Othman.
Tweet