ARSENAL, FRANCE, SKY SPORTS, ARSENE WENGER
THIERRY HENRY

THIERRY HENRY AVAA WIGI

Aliyekuwa mshambulizi mahiri aliyewai kuchezea timu ya Arsenal ya Uingereza na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry aliwashangaza wanafunzi katika shule moja nchini Wales alipoingia darasani akiwa amevalia nywele bandia (maarufu wigi) na miwani na kuwafunza somo la biashara ya ununuzi.

Wanafunzi wa shule ya upili ya Pen-y-Dre ilioko, Merthyr walipigwa na bumbuazi nyota huyo alipojitambulisha kwao kwa niya ya kumkabidhi mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo tuzo la ufanisi katika michezo inayodhaminiwa na shirika la habari la Sky.
Henry, ambaye ni balozi wa masomo wa Sky alimkabidhi Emma Morgan tuzo hilo kwa mchango wake katika michezo. Kipindi hicho cha kuwatuza wanafunzi waliochangia katika michezo katika umri mdogo kitapeperushwa hewani siku ya jumapili katika Sky Sports1.
Emma ambaye amethibitisha udedea wake katika uogeleaji aliweka rekodi ya kuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuiwakilisha Wales katika mashindano ya bara ulaya ya uogeleaji huko Sweden. Emma alimaliza katika nafasi ya pili katika kitengo chake na kutuzwa nishani ya fedha.

LA GALAXY
THIERRY HENRY

Muogeleaji huyo atakuwa miongoni mwa wanaspoti watakaotuzwa siku ya jumapili wakati wa sherehe ya kumtuza mwanaspoti bora nchini Uingereza Wales na Ireland. Henry alisema kuwa Emma alikuwa mwenye ari ya kufaulu na hivyo alistahili tuzo hilo. Mwalimu mkuu wa shule hiyo Keith Maher alisema "kila mmoja wetu alikuwa ameahidi kutotoboa siri hii ya wazo lake Henry mwenyewe kuingia darasani na kujitambulisha kama mwalimu mpya wa Biashara ,,,ilikuwa wazo zuri na limeibua muamkompya miongoni mwa wanafunzi.''
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
  • TANZANIA PORTS AND REVENUE AUTHORITY ON INTER-BANK SETTLEMENT SYSTEM
    The Director of National Payment System at BoT, Mr Bernard Dadi, said the Central bank agreed to extend…
  • MAYWEATHER ATUA DAR ES SALAAM
    Floyd Mayweather Bondia maarufu duniani kwa sasa Floyd Mayweather baada ya kumpiga Emmanuel "Manny"…
  • MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI
    TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI BAADA YA KUGAWANYWA
  • WHY MOBIUS SEEKS NEW MONEY FOR MASS VEHICLE PRODUCTION?
    MOBIUS VEHICLE MANUFACTURE IN KENYA An investor at Mobius says it will sell equity stakes to a number of…
  • ASIJE MTU AKAWAAMBIA MPIGiE KURA YA NDIYO - ASEMA MWANACHAMA WA CCM
    Joseph Butiku, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalim Nyerere “Mchakato huu una mambo makuu mawili ya…
  • WATOTO WAFICHWA NA KUPATIWA MAFUNZO YA KIISLAM KWA SIRI
  • MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAISI ZANZIBAR
    Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha…
  • MUSWADA WA AJIRA WAPITISHWA BUNGENI, TANZANIA
    Bunge la Tanzania Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka…
  • USINUNUE NYUMBA/KIWANJA BILA KUSOMA HIZI SHERIA
    Do not buy Land or House without  reading the following; Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na migogoro…
  • What is the best vehicle manufactured in Afrika? One of them is luxury.
    Kiira EV- interior infront Kiira EV - UGANDA This is a car developed in Uganda by Kiira Motors…

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE