Bwana huyo ambaye taswira yake
akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa
ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza.
Shirika la Habari la BBC
limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi.
Emnuazi ameonekana kwenye
video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa magharibi, akiwemo Mmarekani
James Foley, Raia wa Uingereza, Alan Henning na mwaandishi habari wa Japan,
Kenji Goto.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Yamkini Emnuazi aliyezaliwa
Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29 alikuwa amefahamika sana na
vyombo vya usalama lakini kwa sababu za kiusalama haikuwezekana kumtambua.
Anaaminika amewahi kuishi
Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al
Shabab nchini humo.
Polisi nchini Uingereza
imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari ambazo hawajazithibitisha
kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo bado habari za kina
kumhusu Jihadi John hazijatolewa.
Mwandishi wa maswala ya
Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo vya usalama vya serikali za
mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana kila sababu ya kutahamaki.
Kwa
sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na kundi la
Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na wanamgambo wa Al
Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi
mkubwa
Ishara kuwa Al Shabab
inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda.
Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al
Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria.
Emnuazi ambaye amekuwa
akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata shingo naaminika kuwa mtaalamu
wa maswala ya kompyuta alisomea chuo kikuu cha Westminster.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC
bwana huyo anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya
wakati huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2015/02/150226_jihadi_john_revealed