Santi
Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza
Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.
Ushindi huo wa Arsenal pia
ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi
Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa
penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari
na beki Vincent Kompany.
Arsenal
iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu
uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiwacha City
ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare
ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo
mwezi Septemba.
Tweet