Waziri wa Mawasilaiano, Sayansi
na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa(Mb), akiongea na waandishi wa habari.
Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bwana John Mngodo.
|
Sheria
ya Makosa Mtandao, 2015 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la Serikali la Tarehe
14/08/2015 na kupewa Na.328. Pia Sheria ya Miamala ya Kielektroniki, 2015
ambayo ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe hiyo hiyo na kupewa
Na.329.
Tamko
la kuanza utekelezaji rasmi wa sheria hizo mbili yaani ya makosa ya mtandao ya
mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015
lilitolewa na Wizara ya Mawasilaiano, Sayansi na Teknolojia kupitia waziri
wake, Profesa Makame Mbarawa. Sheria hizo zinaanza kutumika rasmi kuanzia
Jumanne yaani Septemba mosi mwaka huu.
Profesa
Makame Mbarawa, Serikali baada ya kujiridhisha kua maandalizi yote muhimu
ikiwemo elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekelezaji wa sheria hizi
yamefanyika. Sasa, Sheria hizi zitaanza kutumika rasmi tarehe 01/09/2015.
Kwa
hivyo, natoa rain a wito kwa wananchi wote kua tuzingatie “Matumizi Salama na
Sahihi ya Huduma za Mawasiliano na Mtandao kwa manufaa ya kila mmoja na kwa
maendeleo ya Taifa letu. Mitandao ikitumiwa vema ina faida kubwa sana katika
jamii yetu.
Tweet