Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya:
Basili Mramba
Daniel Yona
Gray Mgonja
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu leo imewahukumu kwenda jela miaka
mitatu na faini ya shilingi milioni tano kila mmoja aliyekuwa Waziri wa fedha
Basili Mramba na aliyekuwa Waziri wa nishati na Madini Daniel Yona na kumuachia
huru aliyekuwa Katibu mkuu Wizara ya Fedha Gray Mgonja.
Washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kwa pamoja kuisababishia
serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kwa kuisamehe Kodi Kampuni ya Alex
Stewart ya Uingereza.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua muda mfupi kwa niaba ya jopo la
mahakimu watatu, hakimu Sam Rumanyika amesema washtakiwa hao wametiwa hatiani
pasipo shaka dhidi ya ushahidi wa kuthibitisha makosa yao kutoka upande wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo katika shitaka la kumi na moja la
kusababisha hasara wamepewa adhabu hiyo ya shilingi milioni tano.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mawakili wa utetezi wamedai kukata
rufaa mahakama kuu baada ya kupata nakala ya hukumu.
Shauri hilo limedumu kwa takribani miaka saba tangu wafikishwe
mahakamni hapo mwaka 2008.