Mwanamume mmoja amekutwa na kuondolewa funza wapatao mia moja walio hai tena wanao kula kula puani mwake na kuruhusiwa aende nyumbani .Mwanamume huyo anatajwa kuwa na umri wa miaka sitini na mitano ,na watabibu wanasema funza hao walikuwa wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.
Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.
Na wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu ,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.
Na hali hiyo ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.


Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika
Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.
Iliwachukua siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE