UWAPO MIKONONI MWA POLISI FANYA HAYA 

 1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

 2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali. (Tii Sheria Bila Shuruti)

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

Imetolewa na wakili wetu.

Mshirikishe na mwenzako.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
  • 3 DAYS STATE VISIT TO ISRAEL - UHURU
    President Uhuru Kenyatta is seen off by Deputy President William Ruto President Uhuru Kenyatta left for…
  • OBAMA IN KENYA, RUTO NO SHOW UP
    Obama landing in Kenya Obama in Kenya Ruto no show up The US president was received by President Uhuru…
  • WHO IS ARSENAL FUTURE RIGHT BACK LEGEND?
    Who is Arsenal`s future right back legend? Is he Bellin, Chambers or Debuchy ? Gary Neville was full of…
  • Why People Don't Buy Life Insurance?
    1. It's sold by insurance agents: Let's be honest, most people that sell insurance aren't looked at…
  • 1st MAGUFULI'S CABINET RESHUFFLE
    Mwigulu Nchemba (MP) and Dr. Charles John Tizeba (MP) have been appointed by President John Magufuli of The…
  • How will the Premier League Table be Decided if Two teams Finish Tied at the Top of the Table?
    The pair are not only level on points, but on goals scored, goals conceded, wins, draws and…
  • DANGOTE KUJENGA BANDARI YAKE MTWARA
    Alhaji Dangote akisikiliza maelezo ya eneo husika Mtwara Wakazi wa kijiji cha Mgao, kata Naumbu…
  • WHO ARE WOMEN ELECTED MP'S IN TANZANIA 2015 ELECTION?
    Following the final result that provided a climax to several days of announcement of results for the…
  • 7 OR MORE KILLED BY PARCEL BOMB IN SOUTHERN CHINA
    Guangxi, China. Authorities believe that the bombs were placed in express-delivery parcels, and have asked…
  • AKUTWA NA FUNZA ZAIDI YA MIA MOJA 100
    Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE …

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE