Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam
SULEMAN KOVA akiwaonyesha
wanahabari silaha bunduki 16 zilizokutwa zimefukiwa chini huko pwani mkuranga
huku bunduki 14 zikiwa ni zile zilizoporwa katika shambulio la kuvamiwa kituo
cha polisi stakishari jijini Dar es salaam
Jeshi la polisi nchini Tanzania leo
limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya
kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha
stakshari jijini Dar es salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo
hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kun]kubwa
cha silaha na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na wanahabari
muda huu jijini Dare s salaam kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es
salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi
wema wamefanukiwa kukamata bunduki 16 huku 14 zikiwa ni zile zilizoibiwa katika
tukio la kituo cha staki shari na mbili zikiwa bado hazijulikani ziliporwa kwa
watu gani.
Amesema kuwa zoezi la
kuwasaka watuhumiwa hao lilianza mara baada ya kutokea kwa tukio la stakishari ambapo ilipofika tarehe
17 mwezi huu majambazi hao walijipanga kufanya tukio myinginme maeneo ya
mbagala jijini Dar es salaam ambapo wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la
polisi na wakajipanga tayari kuwakabili.
Hili ndio sanduku lililokua
limehifadhi pesa taslimu million 170 na kufukiwa chini huko mkuranga
Amesema kuwa baada ya
kufika eneo la Twangoma mbagala polisi walijipanga kuwakabili na baadae
majambazi hao walitokea na kuanza kushambuliana na askari hao ambapo katika
mapamano hayo majambazi watano walikamatwa ambapo watatu kati yao walikuwa
tayari wameshakufa na wawili wapo hai hadi leo
Katika taarifa nyingine
ambazo jeshi la polisi kanda maalum ya dare s salaam walizipata jana tarehe
19 ni kuwa kulikuwa na taarifa kutoka
kwa wananchi kuwa kuna tetesi kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha stakishari zilikuwa
zimefichwa katika maeneo ya mkuranga.
Jeshi la polisi waliweka
kambi katika maeneo hayo na kuanza msako maalum wa kuzisaka mahali ambapo
silaha hizo zilikuwa zimefichwa ambapo
katika tukio la kushangaza lilionekana
eneo ambalo lilikuwa limewekwa kinyesi cha binadamu na polisi kupatilia mashaka
na ndipo walipoamua kupachimba na kufanikiwa kupata silaha hizo.
Baada ya kuchimba maeneo
hayo jeshi la polisi lilifanikiwa kukuta silaha aina ambazo ni bunduku aina ya
16 ambazo 14 ni za stakishari,na risasi 55
huku risasi 28 ni zile zilizoibiwa katika tukio la stakishari.
Pamoja na silaha hizo jeshi
hilo lilikuta sanduku kubwa lililokuwa na hela kiasi cha shilingi million
sabini ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani huku KOVA akisema
kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha kamishna kova amesema
kuwa pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado jeshi
la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya kuwasaka
wahalifu hao kwa kuwa bado kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika tukio
la stakishari na bado hazijapatikana.
Tweet