Serikali
ya Jordan imesema itachukua hatua kali za kulipiza kisasi kufuatia kundi la IS
kutoa video inayoonesha rubani wake aliyetekwa na kundi hilo akichomwa moto
hadi kufa. Serikali ya Jordan imesema inajiandaa kumnyonga mwanamke wa Iraq
ambaye kundi la IS lilitaka aachiwe huru. Mfalme Abdullah wa Jordan amelaani
tukio hilo na kulitaja kuwa ni tukio la kigaidi la uoga.
"Katika wakati huu mgumu, ni wajibu wa wajordan
wote kuungana na kuonesha nguvu katika mapambano dhidi ya ugaidi, tukio hili
litatupa nguvu zaidi kupambana na ugaidi."
Mfalme Abdullah ambaye yuko ziarani nchini Marekani
amekatisha ziara yake kutokana na tukio hilo na kurudi nyumbani. Rais Barack
Obama wa Marekani pia alilaani vikali tukio hilo.
"Hili ni moja ya matukio yanayoonesha ukatili na
unyama wa kundi hili, nadhani tutaongeza juhudi na nia yetu kwenye ushirikiano
wa dunia kuhakikisha kundi hilo linashindwa."
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki Moon
amelaani tukio hilo, na kusema kundi la IS halithamini maisha ya binadamu.
Tweet