Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.

Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.

Prissilla alijiunga na shule hii ya 'Leaders Vision Preparatory School' miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.

Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.

Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.

Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake.

Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.

Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.

Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.

Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
  • UHURU IN COURT OVER WAIGURU SAGA
    Raila Odinga is demanding President Uhuru Kenyatta be summoned as a witness in his legal duel with…
  • ALIYEFUNGWA MIAKA 40 BILA KUONANA NA MTU AACHIWA HURU
    Albert Woodfox sasa yuko huru baada ya kuzuiliwa upweke miaka 40 jela Jaji mmoja katika jimbo la…
  • WATOTO WALIOFICHWA WAZUNGUMZA.
    Baadhi ya Watoto 18 Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela…
  • Why we need to have a business of our own?
    This article was inspired by Robert Kiyosaki the author of The Business of the 21st Century and the author…
  • KATIBA INAYOPENDEKEZWA IMEFUTA MAMBO MUHIMU 70 - POLEPOLE ACHAMBUA
  • World's Richest person according to Forbes 2015
    Carlos Slim Helu …
  • NESI AMCHAPA VIBOKO MJAMZITO NA MTOTO AFIA TUMBONI
    MANESI WAKISHIRIKISHANA JAMBO Muuguzi aliyekuwa zamu katika kituo cha Afya cha Muungano wilayani…
  • MUSWADA WA AJIRA WAPITISHWA BUNGENI, TANZANIA
    Bunge la Tanzania Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka…
  • $ 1.9 BLN IN A YR TO BE INVESTED IN ENERGY IN TANZANIA BY 2025
    Dar es Salaam - $1.9 billion to be invested each year in Tanzania by 2025 in energy projects in a bid…
  • 7 OR MORE KILLED BY PARCEL BOMB IN SOUTHERN CHINA
    Guangxi, China. Authorities believe that the bombs were placed in express-delivery parcels, and have asked…

SOCIALIZE

twitterfacebookgoogle plusemail

IN CASE YOU MISSED IT

FOR INSURANCE SERVICES CLICK HERE